Majaliwa kuwabana mawaziri, makatibu wakuu ujenzi mji wa Serikali Dodoma

December 28, 2018 10:16 am · Zahara
Share
Tweet
Copy Link
  • Hatua hiyo inakuja baada ya kutoridhishwa na kasi ya baadhi wakandarasi wanaosimamia ujenzi wa eneo la Mji wa Serikali la Ihumwa Jijini Dodoma ili waeleze kazi hiyo itakamilishwa lini.
  • Awaagiza Wakurugenzi Dodoma kufungua milango kwa vijana kufaidika na fursa za ajira katika mradi huo
  • Wakandarasi walionyeshea kidole ni Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) – Mzinga, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).

Dar es Salaam. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa ameitisha kikao cha Mawaziri na makatibu wakuu wote kesho baada ya kutoridhishwa na kasi ya baadhi wakandarasi wanaosimamia ujenzi wa eneo la Mji wa Serikali la Ihumwa Jijini Dodoma ili waeleze kazi hiyo itakamilishwa lini.

Wakandarasi walionyeshea kidole ni Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) – Mzinga, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).

Ametoa kauli hiyo leo (Desemba 27, 2018) mara baada ya kukagua ujenzi wa ofisi za wizara zote pamoja na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika eneo la Mtumba lililoko kilomita 17 kutoka jijini Dodoma ambapo amesema hajaridhishwa na kazi ya baadhi wakandarasi kutokana na kusuasua kwa ujenzi wa majengo.

“Nimekagua maeneo yote na kukuta baadhi ya wakandarasi wanatakiwa kujenga majengo ya wizara nne hadi tano. Sijaridhika na baadhi ya kazi, nimeitisha kikao cha Mawaziri wote kesho ili tuangalie ni mkandarasi yupi anaweza kumudu hii kazi,” amesema Majaliwa.

Kwa mujibu wa taarifa iliyolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu, kazi hiyo ina malengo maalum na inatakiwa ikamilike haraka sana ili kufikia tarehe ya mwisho ya kukamilisha ujenzi huo iliyotolewa na Rais John Magufuli ya Desemba 31 mwaka huu.

Hata hivyo, amesema sababu ya kukwama kwa ujenzi huo ni kuwepo kwa tatizo la upatikanaji wa vifaa vya ujenzi kama kokoto, nondo, matofali licha ya  uwepo wa watengenezaji wengi wa matofali mkoani humo ambao wakiwezeshwa wanaweza kutengeneza matofali yenye viwango..

“Itisha kikao cha waandishi wa habari uwaeleze wananchi wako fursa zilizopo, kuanzia ufyatuaji wa matofali, uuzaji wa nondo, kokoto na utengenezaji wa “pavement blocks”, hizi zote ni fursa, tuna wizara 24 na mahitaji ni makubwa,” amesema Majaliwa wakati akimuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi ashirikiane na Mkurugenzi wenzake wa Chamwino kuhakikisha vijana wengi wanapata fursa za ajira katika mradi huo.


Zinazohusiana: 


Awali, akitoa taarifa, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Vijana, Anthony Mavunde amesema zoezi la kusafisha eneo la ujenzi wa mji wa Serikali lilianza Novemba 28, mwaka huu na wizara zote zimepata viwanja na zimeanza ujenzi isipokuwa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana) ambao bado wanasubiri kupatiwa fedha.

Kazi ya ujenzi wa Mji wa Serikali inasimamiwa na Kamati ya Kitaifa ya kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
18 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
19 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
19 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Nukta TV

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Nukta TV

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Nukta TV