Magufuli afanya mabadiliko ya uongozi Nec, halmashauri

October 1, 2019 8:26 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Amemteua Dk Wilson Mahera kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).
  • Amefanya uteuzi na kuwahamisha vituo vya kazi baadhi ya Wakurugenzi katika halmashauri mbalimbali nchini. 
  • Uteuzi wa viongozi hao unaanza leo Oktoba 1, 2019. 

Dar es salaam. Raisi John Magufuli amefanya mabadiliko mbalimbali ya viongozi wa Serikali ikiwemo kumteua Dk Wilson Mahera kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Dk Mahera  anachukua nafasi ya mtangulizi wake, Athuman Kihamia ambaye atapangiwa kazi nyingine.  

Kabla ya utezui huo, Dk Mahera alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo (Oktoba 1, 2019) na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, Rais Magufuli pia amemteua Kanali Wilbert Augustine Ibuge kuwa kuwa Balozi na Mkuu wa Itifaki (Chief of Protocal) wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika mashariki.

Kanali Ibuge anachukua nafasi ya Balozi Grace Martin ambaye atapangiwa majukumu mengi ya kibalozi. Uteuzi wa viongozi hao unaanza leo Oktoba 1, 2019.

Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amefanya uteuzi na kuwahamisha vituo vya kazi baadhi ya Wakurugenzi katika halmashauri mbalimbali nchini.  

Wakurugenzi Watendaji wapya

Aliyekuwa katibu Tawala wa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, Ndaki Stephano Muhuli ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro.

Vilevile, Rehema Said Bwasi ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ambapo alikuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga.

Nafasi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro mkoani Morogoro imechukuliwa na Sheillah Edward Lukuba aliyekuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala mkoani Dar Es Salaam. Nafasi hiyo ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala inachukuliwa na Charangwa Seleman Makwiro. 

Mohamed Mavura ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani akitokea Makao Makuu ya Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

Aliyekuwa Afisa Tarafa wa Malangali mkoani Iringa, Ezekiel Henrick Magehema ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyela mkoani Mbeya.


Soma zaidi: 


Naye Afisa Tarafa wa tarafa ya Ukerewe mkoani Mwanza, Diana Sono Zacharia ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama Mkoani Mara.

Dk Magufuli pia amemteua Hanji Godigodi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe, ambapo kabla ya kupata uteuzi huo alikuwa Afisa Elimu Taaluma wa Mkoa wa Dar Es Salaam.

Said H. Magaro ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uyui mkoani Tabora. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Afisa Tarafa wa tarafa ya Msata mkoani Pwani.

Aliyekuwa Afisa Tarafa wa tarafa ya Ifakara mkoani Morogoro Hawa Lumuli, ameteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Malinyi Mkoani Morogoro.

Rais amemteua Afisa Tarafa wa Maswa mkoani Simiyu, Godwin Justine Chacha kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro.

Uhamisho wa Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro, John Kulwa Magalula amehamishwa na kupelekwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Itigi mkoani Singida.

Vilevile, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibiti, Advera Ndebabayo amekwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha.

Katika hatua nyingine, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, MenejImenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni George Mkuchika amefanya uteuzi wa Makatibu Tawala wa Wilaya kama ifuatavyo: 

Charangwa Selemani Makwiro ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala akichukua nafasi ya Sheillah Edward Lukuba aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro.

Vilevile, Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera, Thomas Salala ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Mtwara.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW