Maalim Seif afariki dunia

February 18, 2021 6:32 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amefariki dunia. 
  • Pia alikuwa Mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo.

Dar es Salaam. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amefariki dunia jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi amesema kifo cha kiongozi huyo kimetokea leo Februari 17, 2021 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) majira ya saa 5:00 asubuhi.

Kufuatia kifo hicho, Dk Mwinyi ametangaza siku saba za maombolezo ya kitaifa ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti.

“Taarifa zaidi za msiba huu na maziko yake zitaendelea kutolewa na Serikali kwa ushirikiano wa karibu na familia pamoja na Chama Cha ACT-Wazalendo,” amesema Rais Mwinyi. 

Maalim Seif aliyezaliwa mwaka 1943 kisiwani Pemba, Zanzibar alikuwa Mwenyekiti wa chama cha ACT-Wazalendo. Pia aliwahi kuwa mwanachama wa Chama Cha Wananchi (CUF) na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Rais John Magufuli amesema amepokea kwa masikitiko makubwa kicho cha hayati Maalim Seif na ametoa pole kwa Rais wa Zanzibar na wananchi wote wa Tanzania.

Enable Notifications OK No thanks