M- Pesa, Paypal ilivyotegua kitendawili cha miamala ya kimataifa Tanzania

June 8, 2026 4:15 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Watanzania sasa wataweza kuweka fedha kwenye akaunti zao za PayPal na kutoa fedha kutoka PayPal moja kwa moja kwenda M-Pesa.

Dar es Salaam. Kwa mara ya kwanza nchini Tanzania Kampuni ya Mawasiliano Vodacom kupitia M- Pesa imeingia ushirikiano na kampuni ya malipo ya kimataifa PayPal utakaowezesha wateja kuhamisha fedha moja kwa moja kati ya akaunti zao.

Kupitia mfumo huo mpya, watumiaji wataweza kuweka fedha kwenye akaunti zao za PayPal na kutoa fedha kutoka PayPal moja kwa moja kwenda M-Pesa hatua inayotajwa kurahisisha ufanyikaji wa miamala kimataifa.

PayPal ni kampuni ya kimataifa ya huduma za malipo ya kidijitali inayowezesha watu na biashara kutuma, kupokea na kuhifadhi fedha mtandaoni.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 1998, kampuni hiyo imekuwa ikifanya kazi katika zaidi ya masoko 200 duniani, ikitoa huduma za kutuma, kupokea na kusimamia malipo ya kidijitali kwa watu binafsi na biashara.

Kabla ya kufikiwa kwa makubaliano kati ya kampuni hiyo na Vodacom wafanyakazi, watengeneza maudhui na wafanyabiashara wa mtandaoni walilazimika kutumia njia mbadala zenye gharama kubwa au zinazochukua muda mrefu kutuma au kupokea fedha kimataifa.

Huenda sasa M-Pesa ikawa imetegua kitendawili hicho kwa kuwezesha fedha kutoka kimataifa kuingia moja kwa moja katika mfumo wa fedha wa Tanzania kwa haraka zaidi.

Akizungumzia ushirikiano huo, Kaimu Mkurugenzi wa M-Pesa, Tulisindo Mlupilo alisema hatua hiyo inaakisi dhamira endelevu ya M-Pesa ya kuwaunganisha wateja wake na fursa kubwa zaidi kupitia ubunifu na huduma za kifedha zinazomfikia kila mtu.

“Kuongezeka kwa muunganiko wa kidijitali kunafungua fursa zaidi kwa Watanzania kushiriki katika uchumi wa dunia, iwe kupitia kazi za kujitegemea mtandaoni, biashara za mtandaoni, uundaji wa maudhui au biashara inayovuka mipaka ya nchi,” alisema Mlupilo.

Kwa upande wake mtengenezaji wa maudhui mtandaoni, Rosemary Julius Majengo ameieleza Nukta Habari kuwa kwa sasa imekuwa rahisi kutoa fedha anazolipwa kutoka kwenye majukwaa ya kidijitali, hatua iliyopunguza changamoto za upatikanaji wa mapato yake aliyopata mtandaoni.

“Zamani ilikuwa pesa inaingia unabaki kuiangalia tu kwa sababu huwezi kuitoa, lakini saivi unaweza ku ‘Integrate’ na M-pesa na kutoa mapato yako,” ameeleza Majengo.

Fursa kwa ‘gig economy’

Wakati Vodacom na PayPal wakikamilisha ushirikiano huo, takwimu za kimataifa zinaonyesha kuwa uchumi wa kazi za mtandaoni (gig economy) unaendelea kukua kwa kasi hatuia inayotajwa kuwa fursa. 

Kwa Tanzania, fursa hiyo imekuwa ikikua sambamba na kuongezeka kwa matumizi ya intaneti na simu janja ambazo kwa mujibu wa takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), kufikia Machi 2026 zimefikia idadi ya milioni 29.8.

Hata hivyo, Watanzania wengi walikuwa wakikosa fursa hizo za kazi za mtandaoni kutokana na kukosekana kwa mfumo maalumu wa malipo unaotambulika kimataifa. 

Kupitia uunganishwaji wa Paypal na M-Pesa, Watanzania wanaopata mapato kupitia majukwaa ya kimataifa wanaweza kupata fedha zao kwa urahisi zaidi na kuzitumia moja kwa moja katika shughuli za kila siku, jambo linaloweza kuongeza mzunguko wa fedha ndani ya uchumi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
8 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
8 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Nukta TV

Tunachokifahamu kuhusu ziara ya Rais Samia Urusi, kidiplomasia na uchumi

Tunachokifahamu kuhusu ziara ya Rais Samia Urusi, kidiplomasia na uchumi

Nukta TV

Kutoka Ubunge hadi mshauri wa Rais, Panda shuka ya Ummy Mwalimu katika siasa

Kutoka Ubunge hadi mshauri wa Rais, Panda shuka ya Ummy Mwalimu katika siasa

Nukta TV