Lissu akutwa na kesi ya kujibu, akitaja mashahidi 11

August 21, 2026 1:33 pm · Lucy Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Uamuzi huo, uliotolewa na Jaji Dunstan Ndunguru kwa niaba ya majaji wenzie wawili, ni pigo kwa Lissu ambaye sasa atatakiwa kuwaleta mashahidi wake 11 kujitetea.

Dar es Salaam. Mahakama Kuu ya Tanzania imemkuta Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Lissu na kesi ya kujibu katika mashtaka ya uhaini yanayomkabili, hatua itakayomfanya aendelee tena kusota mahabusu huku akijitetea kujinasua katika shtaka hilo.  

Uamuzi huo, uliotolewa na Jaji Dunstan Ndunguru kwa niaba ya majaji wenzie wawili, ni pigo kwa Lissu ambaye sasa atatakiwa kuwaleta mashahidi wake 11 kujitetea ili aweze kuepuka na kesi hiyo ambayo iwapo atakutwa na hatia hukumu yake ni kifo. 

Hatua ya uamuzi wa leo katika Mahakama Kuu ya Tanzania masjara ndogo ya Dar es Salaam imekuja baada ya upande wa mashtaka kufunga ushahidi wake Jumatatu hii kwa kuwasilisha ushahidi wa mashahidi 17 kati ya 30 waliotarajiwa.

Jaji Ndunguru amesema leo Agosti 21, 2026 kuwa kutokana na mapitio ya ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka na hoja zilizotolewa na mshtakiwa wameona ana kesi ya kujibu. Lissu amekuwa akijitetea katika kesi hiyo inayofuatiliwa zaidi ndani na nje ya nchi kutokana na kumhusisha kiongozi huyo wa juu wa chama kikuu cha upinzani nchini. 

Lissu, ambaye aliyekamatwa Aprili 9 mwaka jana, ameshatimiza takriban siku 500 akiwa mahabusu. Anashtakiwa kwa kosa la uhaini kinyume na Sheria ya Kanuni ya Adhabu iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2023 linalotokana na tuhuma za matamshi aliyoyatoa Aprili 3, 2025 jijini Dar es Salaam ya kutoshiriki na kuzuia Uchaguzi Mkuu 2025. 

Lissu amesema upande wa utetezi unapendekeza mashahidi 11 wakiwemo Rais Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais mstaafu, Dk Philip Mpango na vigogo wengine wa Chadema ambao utaomba mahakama iwape ‘summons’ (wito) kwa ajili ya ya kutoa ushahidi kuhusu masuala mbalimbali yanayohusiana na kesi. 

“Upande wa utetezi unaamini (Samia Suluhu Hassan) anaweza kutoa ushahidi kuhusu masuala yanayohusiana na Serikali, pamoja na nafasi yake kama Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Taifa na taarifa alizonazo kuhusu matukio yanayodaiwa katika kesi hii,” amesema Lissu akimwelezea shahidi wa kwanza Rais Samia. 

Mashahidi wengine wanaotarajiwa kutoa ushahidi huo kwa ajili ya utetezi ni Katibu Mkuu wa Chadema John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu Bara Amani Golugwa, Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS), na Mkurugenzi wa Mawasiliano, Brenda Rupia. 

Katika maelezo yake, Lissu ameielezea mahakama juu ya tatizo la kuzuiwa mawakili na mashahidi wake na kwamba anaamini kuwa wakati utakapofika kuandaa utetezi wake Mahakama itahakikisha kwamba anapata fursa ya kufanya hivyo kikamilifu. 

“Kwa hiyo, naomba waheshimiwa majaji mtoe amri itakayoniwezesha kukutana na kushauriana na mashahidi wangu kwa faragha, bila kusikilizwa au kufuatiliwa na watu wengine, wakiwemo maafisa wa magereza au maafisa wengine wa Serikali,” amesema Lissu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
21 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
EXCLUSIVE: Namna sahihi ya kunyonyesha baada ya kujifungu | Part 2

EXCLUSIVE: Namna sahihi ya kunyonyesha baada ya kujifungu | Part 2

Nukta TV

EXCLUSIVE | TEASER | Namna sahihi ya kunyonyesha baada ya kujifungua

EXCLUSIVE | TEASER | Namna sahihi ya kunyonyesha baada ya kujifungua

Nukta TV

RC Chalamila: Hii ni vita, hakuna hata mmoja wakucheza na uhai wangu

RC Chalamila: Hii ni vita, hakuna hata mmoja wakucheza na uhai wangu

Nukta TV