LHRC yahimizwa kuimarisha mifumo ya Tehama
- Tehama itasaidia LHRC kutoa msaada wa kisheria katika maeneo mengi zaidi nchini.
- Mfumo dume kwa wanawake watajwa kuwakosesha haki za kisheria.
Dar es Salaam. Mkurugenzi wa idara ya haki za binadamu Wizara ya Katiba na Sheria Nkasori Sarakikya, amekitaka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kuimarisha mifumo ya Teknolojia, Habari na Mawasiliano (Tehama) ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za kisheria katika maeneo mengi nchini.
Sarakikya aliyekuwa akizungumza leo August 20, 2024 jijini Dar es Salaam katika hafla ya uzinduzi wa ripoti ya LHRC kuhusu msaada wa kisheria kwa mwaka 2023 amesema kuwa matumizi ya teknolojia ya kisasa yatarahisisha upatikanaji wa haki za kisheria kwa wakati na usawa kwa makundi yote.
โKuanzishwa kwa mfumo wa usimamizi wa msaada wa kisheria kuliboresha kwa kiasi kikubwa kurekodi na kufanya ufuatiliaji wa kesi za wateja na hivyo kuchangia kuongezeka kwa ufanisi wa huduma zinazotolewa na kituo hikiโฆ
โฆNiwasihi mueendelee kupanua wigo wa upatikanaji haki kwa makundi yote na kuimarisha mifumo ya Tehama ili kufikia wananchi wengi hususan wanaoishi maeneo ya pembezoni,โ amesema Sarakikya.
Matumizi ya Tehama ni miongoni mwa masuala yanayohimizwa sana na viongozi mbalimbali nchini siku za hivi karibuni kutokana na maendeleo ya sayansi na teknolojia pamoja na umuhimu wake katika kurahisisha kazi.
Miongoni mwa viongozi hao ni Rais Samia Suluhu Hassan ambaye Oktoba 23, 2023 aliwataka majaji kutumia teknolojia ya kisasa katika usikilizaji wa mashtakia ili kurahisisha upatikanaji wa haki.
Kupitia mifumo hiyo ya Tehama huenda vituo vya utoaji wa msaada wa kisheria ikiwemo LHRC vikapanua wigo wa utoaji wa huduma ikiwemo kuwafikia wananchi walioko katika maeneo ambayo huduma ya msaada wa kisheria ni ngumu kufikika.
Mathalan mwaka 2023 LHRC ilitoa huduma ya msaada wa kisheria mikoa yote ya Tanzania isipokuwa mikoa ya Katavi na Sumbawanga huku ikisaidia wananchi 30,000.
Miongoni mwa mashtaka yaliyoripotiwa zaidi kwa mujibu wa ripoti hiyo ni yale yaliyohusu familia, migogoro ya ardhi, jinai, talaka, mirathi na matunzo ya watoto.

Wajumbe waliohudhuria mkutano wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Anna Henga aliyekuwa akizungumza katika uzinduzi wa Ripoti ya Msaada wa Kisheria / Picha LHRC.
Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC Anna Henga aliyekuwa akizungumza katika uzinduzi wa ripoti hiyo amesema bado kuna mwitikio mdogo wa wanawake kuripoti changamoto zao katika vituo vya msaada wa kisheria.
Kwa mwaka 2023 ni asilimia 35 tu ya wanawake ndiyo waliohudumiwa na kituo hicho kulinganisha na asilimia 65 ya wanaume huku mfumo dume ukitajwa kuwa sababu.
โLakini pia mfumo dume umewagandamiza sana wanawake hata wakifanyiwa ukatili wanaona ni sawa, lakini sababu nyingine ni kuwa wanawake hawamiliki mifumo rasmiโฆ
โฆWanakuwa hawapo kwenye ajira rasmi, ardhi wanayomiliki wanawake inakuwa ya kutumia tu ni ardhi ya baba yake, baba mkwe, mume wake, wakwe kwa hiyo anakuwa hana hiyo kesi ya ardhi kwa kuwa hana hiyo ardhi yenyewe,โ amebainishaย Henga
Ili kutatua changamoto hiyoย LHRC imeanzisha utaratibu wa kuwafuata wanawake walipo na kuwafikia moja kwa moja ili kuwapa elimu zaidi.
โKwanzia mwaka jana tumeamua kwenda walipo wanawake kama ni masokoni, hodi za mateneti na kwingine ili tuwafikie moja kwa moja lakini pia tulikwenda magerezaniโฆ.
โฆChangamoto pia ya magerezani wanawake ni asilimia tano tu ya wafungwa lakini hiyo asilimia tano tuliwafikia wote hata wale ambao kesi yake imeshaisha tulimpa elimu,โ ameongeza Henga.
Latest
