Kwanini inachukua muda mrefu kushuka kwenye ndege baada ya kutoa ‘Airport’

May 20, 2019 3:15 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Wakati mwingine, watu hawaruhusiwi kutoka mapema kwenye ndege kutokana na changamoto za kiufundi ambazo zinaweza kutokea kwenye ndege au uwanjani. Picha|Mtandao.


  • Baadhi ya sababu hizo ni ukamilishaji wa mawasiliano ya usalama kati ya rubani na wafanyakazi wa airport.
  • Kutua kwa ndege nyingi kwa wakati mmoja, pia ni sababu nyingine.

Kama unatumia usafiri wa ndege, utakuwa umejenga tabia ya uvumilivu na subira kutokana na mchakato wa usalama unaotakiwa kuufuata kabla na baada ya kusafiri. 

Kuanzia unapokaguliwa mizigo na hati za kusafiri, unapoingia ndani ya ndege lakini hadi unashuka katika kiwanja cha ndege ni mchakato mrefu ambao unahitaji muda wa kutosha ili kuhakikisha kanuni na taratibu za usafiri huo zinazingatiwa kama zilivyopangwa. 

Lakini lipo jambo moja ambalo baadhi ya wasafiri wamekuwa wakikosa nalo uvumilivu ambalo ni wakati wa kushuka kwenye ndege. Wengi hutamani kuona ndege inapotua tu kwenye kiwanja cha ndege “Airport” washuke mara moja lakini inakuwa tofauti. 

Huenda hali hiyo imewahi kukuta na umebaki na maswali mengi yasiyokuwa na majibu. Hizi ndizo sababu kwanini ndege ikitua airport huchukua muda kwa watu kuruhusiwa kutoka ndani ya ndege:-

Kwanza ndege ikitua, rubani husubiri kwa muda kidogo ili injini itulie na kuwapa ishara wafanyakazi waliopo uwanjani ambao hutathmini hali ya usalama wakati kama inaruhusu milango ya ndege kufunguliwa. 

Wakati huo abiria kwenye ndege husimama na kuweka mizigo ya tayari na wahudumu wa ndege nao wakikamilisha hatua zilizobaki ikiwemo kuwasiliana na chumba cha marubani. 


Zinazohusiana:


Baada ya mawasiliano ya rubani na wafanyakazi wa ‘aiport kukamilika, ngazi ya kushukia (jet bridge) husogezwa hadi kwenye mlango wa ndege na kuwapa ishara wahudumu wa ndege kuufungua mlango ili watu watoke nje. 

Wakati mwingine, watu hawaruhusiwi kutoka mapema kwenye ndege kutokana na changamoto za kiufundi ambazo zinaweza kutokea kwenye ndege au uwanjani. 

Lakini kutua kwa ndege nyingi kwa wakati mmoja, pia kunaweza kuchelewesha watu kutoka kwenye ndege hasa kama uwezo wa wafanyakazi wa airport ni mdogo kusimamia ndege zote kwa wakati mmoja. 

Sababu nyingine ambayo haina nguvu ni changamoto za kibinadamu ambazo zinaweza kutokea wakati wa usimamiaji wa majukumu ya airport. Mfano wafanyakazi wa  uwanja wa ndege wanaweza kupitiwa au kuchanganya muda wa ndege kutua na wakaendelea shughuli nyingine. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV