Karibu robo ya wanafunzi hawajaripoti kidato cha kwanza Tanzania

February 13, 2023 7:29 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Hadi Februari 10, wanafunzi 915,919 kati ya milioni 1.07  walikuwa wameripoti shuleni.
  • Serikali yawataka wazazi kuwapeleka shuleni watoto ambao hawajaripoti bado kabla haijachukua hatua. 

Mwanza. Karibu robo ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza Tanzania bado hawajaripoti shuleni huku Serikali ikiwataka wazazi kuwapeleka mara moja kabla hatua zingine hazijachukuliwa.

Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza Februari 12, 2023, amesema wanafunzi milioni 1.07 walichaguliwa kujiunga kidato cha kwanza mwaka huu lakini hadi kufikia Februari 10 ni wanafunzi 915,919 walikuwa wameripoti shule.

Hiyo ni asilimia 85.34 ya wanafunzi wote waliochaguliwa au sawa na kusema wanafunzi nane kati ya 10. 

“Kwenye kidato cha kwanza kulikuwa na shida kidogo wakati tunaanza walioriopoti walikuwa wachache lakini sasa angalau wanaendelea kuripoti, nitoe wito kwa wanafunzi ambao hawajaripoti kuhakikisha wanaenda kwa kuwa Serikali imeboresha miundombinu ya kujifunzia,” amesema Msigwa.

Amesema Serikali imejenga vyumba vya madarasa na kuweka madawati kwa shule zote za sekondari nchini, ingawa kuna changamoto ya upungufu wa walimu lakini inajitahidi kuhakikisha suala hilo linatafutiwa ufumbuzi.

Amesema wameweka mfumo wa kufuatilia wanafunzi wote waliofaulu na kupangiwa kwenye shule zao. Iwapo mwanafunzi hatakuwa ameonekana katika shule aliyopangiwa kwa muda wa siku 21 atahesabika kuwa ni mtoro au ameacha shule na mfumo utamuondoa.


Soma zaidi:


Amesema kwa wanafunzi wanaopelekwa shule za binafsi, serikali pia imetoa maelekezo kwa shule hizo kuhakikisha zinapeleka taarifa hizo kwenye mfumo ndani ya siku 90 iwapo hazitafanya hivyo mwanafunzi ataondolewa kwenye mfumo na kuhesabika kuwa ni mtoro.

“Hivyo tunawaomba wazazi wote kuhakikisha wanawapeleka watoto wao shule na wale waliowapeleka shule binafsi tupate taarifa zao ili ziweze kujumuishwa,” amesema Msigwa.

Tunaboresha elimu

Amesema kupitia fedha za mradi wa Uviko-19, jumla ya vyumba vya madarasa 15, 000 vilijengwa lakini pia serikali ilitoa zaidi ya Sh160 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 8,000.

Msigwa amesema mwaka huu Serikali imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 9,000 kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la awali na msingi.

“Tunataka watoto wanapoingia madarasa ya awali na msingi wasipate shida ya sehemu ya kujifunzia kwa kuwa Serikali inaendelea kutoa fedha ili kuboresha miundombinu ya kusomea,” amesema Msigwa.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
7 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
7 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

MFUMUKO WA BEI kuendelea kuwa mdogo licha ya gharama za mafuta

Nukta TV

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Hali ya uchumi Tanzania: Makadirio ya ukuaji wa uchumi Bara 6%, Zanzibar 6.6%

Nukta TV

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

BoT: Yatangaza ongezeko la riba ya Benki kuu hadi 6.25%

Nukta TV