Kambi mpya kuzinduliwa hifadhi ya Taifa ya Serengeti Julai

April 26, 2019 4:00 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link

Muonekano wa kambi hiyo ya Nimali Mara itakayozinduliwa Julai mwaka huu. Picha|Mtandao.


  • Itakuwa na mahema na huduma muhimu kwa ajili ya watalii na wanandoa wanaopendelea kupiga kambi katika hifadhi za Taifa. 
  • Inapatikana katika eneo la Kogatende lilipo kaskazini mwa hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Dar es Salaam. Kama una mpango wa kutembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti katika robo ya pili ya mwaka 2019 na unakusudia kupiga kambi katika hifadhi hiyo, basi watoa huduma wamekurahisishia sehemu nzuri ya kupumzika na uwapendao. 

Kampuni ya Nimali Africa inayotoa huduma za utalii inakusudia kuzindua kambi mpya ya Nimali Mara katika eneo la Kogatende lilipo kaskazini mwa hifadhi ya Taifa ya Serengeti mnamo Julai mwaka huu.

Kambi hiyo itakuwa ina vyumba nane na viwili kwa ajili ya mapumziko ya wanandoa (honeymoon) ambapo kila kimoja kitakuwa na bwawa la kuogelea na eneo la mapumziko ya familia. 

Kwa mujibu wa kampuni hiyo, kambi hiyo ambayo itafunikwa vizuri kwa mahema ambayo yatakuwa na milango ya mbao, mabafu yenye na majakuzi ya kuogea (bath tub). Pia kila hema litakuwa na huduma muhimu zinazohitajika kwenye nyumba ikiwemo viti, kitanda na majiko ya nje kwa ajili ya kupikia. 


Zinazohusiana:


Ukiwa katika kambi ya Nimali Mara utapata fursa ya kucheza michezo mbalimbali, safari za maputo (hot-air ballon safaris), kuangalia ndege na nyani, kupata kifungua kinywa cha porini na aina mbalimbali ya vyakula. Kama unataka matembezi nayo unaweza kuyapata.

Kambi hiyo huenda ikasaidia kuongeza mapato yatokanayo na kodi ikizingatiwa kuwa watalii watapata huduma za karibu na hifadhi na hivyo kutumia fedha zao katika eneo hilo.

Nimali Mara itakuwa kambi ya tatu inayomilikiwa na kampuni ya Nimali Africa. Kambi zingine ni Nimali Tarangire ambayo iko katika Hifadhi ya Taifa ya Tarangile na Nimali Central Serengeti  ambayo iko katika uwanda wa kaskazini wa Serengeti karibu na kilima cha Makoma.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV