Kamanda Muliro aondoka Mwanza na tukio lisilosahaulika

June 2, 2021 5:57 am · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni Kamanda Jumanne Muliro aliyehamishiwa Mkoa wa Dar es Salaam.
  • Anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Camilius Wambura aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).
  • Amesema hatasahau tukio la kizushi la kukamatwa kwa vichwa 20 vya watoto katika kituo cha polisi Nyakato.

Mwanza. Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro aliyehamishiwa Mkoa wa Dar es Salaam amesema hatasahau tukio la kizushi la kukamatwa kwa vichwa 20 vya watoto katika kituo cha polisi Nyakato mkoani humo, jambo lililoibua taharuki kubwa kwenye jamii.

Kamanda Muliro anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Camilius Wambura ambaye amepandishwa cheo na kuwa Kamishna wa Polisi na kuteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Amesema tukio hilo lilitokea Februari  20, 2019 ambapo waandishi wa habari walilipoti taarifa hiyo bila kuwa na uhakika wa tukio lenyewe, jambo lililomuweka katika wakati mgumu kiuetendaji.  

“Ni nitukio ambalo lilitengeneza taharuki kwa wananchi na hata vyombo vya dola vilitahamaki, lakini tunashukru uongozi wa waandishi wa habari mkoa wa Mwanza tulikaa pamoja kuhakikisha suala hilo linatatuliwa,”amesema Kamanda Muliro.

Amesema tukio lilikuwa siyo la kweli na kulikuwa hakuna taarifa za kutosha.  


Soma zaidi: 


Hata hivyo, Kamanda huyo amewashukuru waandishi wa habari kwa kuwa sehemu ya kazi yake na kwamba wamemsaidia katika kuibua matukio mengi na kumpatia taarifa kwa ajili ya ufuatiliaji mkoani humo.

“Waandishi wa habari kwangu wamekuwa kama mbwa wanaobweka pale wanapoona kuna hatari yaani “watch dog”, wamenisaidia sana  katika mfumo wa utendaji kazi na pia wamechangia katika kuufanya Mkoa wa Mwanza kuwa tulivu,” amesema. 

Enable Notifications OK No thanks