Jinsi ya kubaini picha zinazopotosha kuhusu Corona mtandaoni.

May 12, 2020 12:43 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Itakuwezesha kujua picha hiyo ilichapishwa kwa mara ya kwanza lini na tovuti au mtandao gani.
  • Pia imetumika mara ngapi mtandaoni.
  • Kama picha unayotafuta haijawahi kutumika mtandaoni, haitaonekana.

Dar es Salaam.Kumekuwa na wimbi kubwa la kusambaa kwa habari nyingi za uzushi ambazo mara nyingi vyanzo vyake huwa ni picha au video.

Tatizo hilo limesambaa ulimwenguni kote ikiwemo nchini mwetu Tanzania, lakini juhudi mbalimbali zinafanyika za kukabiliana na habari ikiwemo kujifunza nyenzo za kidijitali kama “Google Images” ni muhimu kuweka ukweli wazi.

Leo tungependa tujifunze zaidi naamna ya kuweza kuthibitisha habari picha zilizopo kwenye mitandao ya kijamii zinazodaiwa kuwa ni tukio la kweli lakini kiuhalisia ni uzushi kwa kutumia Google Images.

Hatua ya kwanza, mara baada ya kupata picha ama kutoka katika mitandao ya kijamii au uliyoitilia shaka ni kwenda kwenye mtandao wa Google kisha tafuta neno ‘Google Images’.

Baada ya  kutafuta hiyo, hatua ya pili utaona sehemu yako ya kutafuta taarifa yako imekuwa tofauti kidogo kitafutio cha kawaida cha Google.Hapo utaona imeandikwa Google Image na sehemu ya kutafutia taarifa kuna alama tatu ambazo ni alama ya picha, kipaza sauti na sehemu ya kutafutia.

Hatua ya tatu utatakiwa kuweka picha yako (Uplod you Image) kwa kubonyeza kitufe cha kamera ambapo utaona dirisha dogo limefunguka likiwa na taarifa  ‘Search by image”.
Search Google with an image instead of text. Try dragging an image here.’  yenyewe maana ya tafuta picha, tafuta kwenye Google kwa kutumia picha badala ya maneno. Jaribu kuiweka picha hapa’

Baada ya hapo atatakiwa kuweka picha hiyo kwa njia mbili ama kuweka kutumia kiunganishi (Paste image URL) au kuipandisha picha hiyo (Upload an Image) kutoka mtandaoni au kwenye kompyuta yake.


Zinazohusiana:



Hatua ya nne baada ya kuipandisha picha hiyo kwenye mtandao wa Google Image ataweza kuiona picha hiyo ikileta majibu  endapo tu itakuwa imeshawahi kuchapishwa kokote pale mtandaoni. Lakini kama haijawahi kuchapishwa kwenye mtandao haitaleta majibu yoyote.

Majibu hayo katika Google Image huwa yanaonekana katika hatua tatu, matokeo ya kwanza ni maelezo kuhusu picha hiyo, matokeo ya pili  ni yale yanayoonyesha picha zinazofanana na hiyo utakayokuwa unaitafuta mtandaoni kama ipo (Visually similar images).

Matokeo ya tatu  ni yale yanayoonyesha  kama picha  hiyo imeshawahi  kutumika sehemu nyingine yoyote. Katika matokeo hayo utaweza kupata  taarifa ya picha hiyo imechapishwa mara ngapi, wapi na chombo gani cha habari na imechapishwa lini kwa mara ya kwanza.


Hivyo basi kama ukiweza kutumia Google Image vizuri itakuwa rahisi kuepuka kusambaza taarifa za uongo mtandaoni na utakuwa umeiokoa jamii kutokana madhara ya habara za uongo hasa katika kipindi hiki cha janga la Corona.

Enable Notifications OK No thanks