Jinsi ya kuandaa mkate wa tangawizi

December 5, 2024 2:50 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • ulaji wa mkate husaidia kuboresha mmeng’enyo wa chakula,pamoja na unyonyaji wa virutubishi ulioimarishwa.

Inawezekana umewahi kula aina tofauti za mikate ukiwemo wa jibini, ngano, ndizi, mchele na aina nyingine.

Kitafunwa hiki sio tu kina nzuri lakini kina faida nyingi za kiafya ikiwemo kuongeza virutubisho kwenye mwili kama wanga, protini, vitamini B6, B12, nyuzi nyuzi, pamoja na madini ya selenium, manganezi, fosforazi, shaba na foleti.

Kwa mujibu wa tovuti ya Medicover Hospitals, ulaji wa mkate husaidia kuboresha mmeng’enyo wa chakula, pamoja na unyonyaji wa virutubishi ulioimarishwa.

Basi leo ngoja tujifunze kuandaa mkate wa tangawizi, ambapo kwa baadhi ya watu hupendelea kutumia katika mapishi hususan ya vinywaji kama chai.

Namna ya kuandaa hatua kwa hatua

Hatua ya kwanza katika bakuli kubwa weka unga wa ngano ambao haujakobolewa, unga wa ngano uliokobolewa, chumvi, tangawizi, mdalasini, baking powder na baking soda, maziwa, mayai, mtindi, mafuta ya kupikia na vanilla, kisha changanya mchanganyiko huo. Unaweza kutumia mashine ya kuchanganyia ama mikono kwa dakika 15 hadi 20.

Baada ya hapo chukua sufuria la kuoka mkate, tanguliza karatasi ya kuokea na mimina mchanganyiko wote uliochanganya kwa kutumia mashine ya kuchanganya ndani ya sufuria la kuoka mkate.

Hatua inayofuata ni kuandaa jiko la kuokea mkate. Kwa wale wanaotumia jiko la kisasa la kuokea weka joto la nyuzi 175° C  kisha acha jiko lipate moto.

Jiko likishapata moto, weka sufuria la kuoka mkate, na uoke kwa muda wa dakika 40 mpaka 45, au hadi utakapo ona mkate umeiva na kuwa na rangi ya kahawia.

Baada ya dakika 45 utakuwa umesha iva uondoe kwenye jiko la kuoka, kisha uweke pembeni ili upoe, ukiwa bado ndani ya sufuria.

Mpaka hapo mkate wako utakuwa tayari kwa kuliwa unaweza kuula kwa kutumia chai ya maziwa ,viungo ama juisi ni wewe tu utakavyopenda.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV