Maandalizi ya mchanganyiko wa tangawizi na kitunguu swaumu 

January 14, 2024 1:46 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Huokoa muda na usumbufu wa kuandaa viungo hivyo ara kwa mara.
  • Mchanganyiko huu unaweza kukaa kuanzia wiki tatu na kuendelea bila kuharibika.
  • Ni chanzo kizuri cha kujiingizia kipato.

Tangawizi na kitunguu swaumu ni miongoni mwa viungo muhimu katika mapishi  ya kila siku, uwepo wake katika mboga huongeza ladha na harufu nzuri inayovutia.

Licha ya umuhimu wake katika mboga, kuandaa viungo hivi kila siku huchosha hususan kama unapika chakula cha watu wengi kinachohitaji viungo hivyo.

Habari njema ni kwamba unaweza kutengeneza mchanganyiko wa viungo hivyo ukavihifadhi kwa muda mrefu wa zaidi ya wiki tatu na kuokoa gharama pamoja na muda wa kuviandaa kila siku.

Mchanyiko huu pia unaweza kuwa biashara itakayokuingiza kipato kuanzia 2500 mpaka Sh5000 kutengemea na vifungashio utakavyotumia. 

Karibu jikoni tujifunze na tuandae kwa pamoja mchanganyiko wa tangawizi na kitunguu swaumu.

Jinsi ya kutengeneza 

Osha tangawizi, menya na uzikate  vipande vidogo  vidogo weka kwenye bakuli kisha hamia kwenye kumenya vitunguu swaumu, ongeza chumvi kiasi  tayari kwa  ajili ya kusaga.

Katika hatua hii unaweza kusaga kwa kutumia blenda ya umeme, kisagio cha mkono au kutwanga na kinu,cha muhimu viungo vyako vilainike vizuri. 

Kama unatumia blenda ya umeme au kinu ongeza maji, mafuta na ‘vinegar’ wakati unasaga aukutwanga ili kusaidia viungo kulainika kwa urahisi na kukaa kwa muda mrefu bila kuharibika.

Unaweza kuongeza viungo zaidi kama kotmiri na vinginevyo katika mchanganyiko wako ili kuonngeza ladha na harufu nzuri.

Viungo vikisagika vizuri mchanganyiko wako utakuwa tayari kwa kutumiwa.

Kinu kidogo kinaweza kusaidia kutengeneza mchanganyiko wa kitunguuswaumu na tangawizi.Picha|The paste.

Mambo ya kuzingatia

Ili mchanganyiko huu uweze kudumu kwa muda mrefu ni lazima uhifadhi kwenye friji au kama utatumia njia ya kawaida basi tumia chombo chenye mfuniko usiopitisha hewa.

Hakikisha unatumia mafuta, chumvi na ‘Vinegar’ ya kutosha ikiwa hautumii friji kuhifadhi ili viungo vyako viweze kudumu kwa muda mrefu zaidi.

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Unaweza kusema ni maumivu juu ya maumivu kwa watumiaji wa vyombo vya moto vinavyotumia mafuta ya

Nukta TV

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Neema Mohamed, Mkurugenzi wa Bone and Blood Foundation, ni shujaa wa ugonjwa wa selimundu Sickl

Nukta TV

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ametua kwenye ardhi ya Urusi kwa ziara ya kitaifa ya siku

Nukta TV