Jinsi InVID inavyotumika kung’amua video za uzushi

July 5, 2020 12:32 pm · Daniel
Share
Tweet
Copy Link
  • Mtumiaji ili aweze kuitumia  InVID atatakiwa kupakua kwanza kiunganishi cha InVID (InVID plugin).

Dar es salam. Ukuaji wa teknolojia ya habari na mawasiliano ume chochea kuongezeka kwa mahitaji ya habari kiasi cha kuchangia ongezeko la habari za uongo ulimwenguni hususan wakati huu wa janga la corona.

Janga hilo la habari za uzushi limefanya kuwe na jitihada nyingi za kusaidia kupunguza ueneaji wa habari hizo kupitia zana mbalimbali za kijigitali ikiwemo InVID inasaidia kubaini video za uzushi.  Programu hii ilikuwa inafadhaliwa na Umoja wa nchi za Ulaya.

Kupitia makala hii tungependa tujifunze namna ya kutumia InVID kuthibitisha kama video iliyotumika katika habari fulani ni ya kweli au ya ‘kupikwa’ kiasi kwamba haiendani hata kidogo na habari yenyewe.

Ili uweze kuitumia InVID kama mwanahabari au mtu yoyote unatakiwa uwe na kompyuta  ambayo ina kitafutio cha Google Chrome  ili uweze  kuitumia kupata kiunganishi ( InVID plugin).


Hakikisha umeipakua InVID kwenye kompyuta yako

Hatua ya kwanza ni kuipakua  zana hiyo kupitia kiunganishi (InVID plugin) kwa kufuata maelekezo yote. Ukishaipata na kuifungua utakutana na neno lilokolezwa kwa rangi ya bluu “Add to Chrome”.  Utatakiwa kubonyeza hapo kisha utakuwa umefanikiwa kuwa nayo kwa ajili ya kuanza kuitumia.

Baada ya kuipakua, InVID itakuwa upande wa kulia wa juu wa kompyuta yako ikionekana kwa maandishi meusi yaliyozungukwa na rangi nyeupe.

Jinsi InVID inavyofanya kazi

Mwandishi wa habari au mtumiaji yoyote utakapoamua  kutumia InVID katika kuthibitisha habari utatakiwa kubonyeza zana hiyo ambayo ipo upande wa juu kulia.

Baada ya kubonyeza utaona machaguo matatu ambayo ni kufungua InVID(Open InVID), viunganishi vya video (Video urls) na viunganishi vya  picha (Image urls).

Jinsi ya kuanza kuthibitisha Video

Katika hatua hii utatakiwa kuchagua chaguo la kwanza ambalo ni  InVID (Open InVID).

Baada ya kubonyeza kipengele hicho itakuhamisha kwenda kwenye kipengele kingine ambacho utaona zana mbalimbali  ndogo ndogo zilizopo ndani ya InVID.

Hatua hiyo itakuwezesha kutumia zana hizo ndogo ndogo zilizopo ndani ya InVID  kutokana na mahitaji yako.

Mathalani kupitia dhana ndogo ya “Keyframes” iliyopo ndani ya InVID utaweza kujua video unayotaka kuithibitisha imetumika lini na wapi au kama kuna picha tofauti imeongezwa zaidi ya zile za asili. Watengenezaji wa habari za uzushi kwa njia za video hutumia sana njia hii kuongeza kipande au sauti kwenye video ya awali ili kuhadaa watu.

Mtumiaji wa InVID utatakiwa kubonyeza  “Keyframes” kisha itakupeleka kwenye eneo ambalo utaweza kuweka  viunganishi vya video( linki ya video ) husika au kama hana  kiunganishi utaweza kuipandasha video kutoka  kwenye kompyuta yake.

Fursa hiyo itakuwezesha kuweka video hiyo kwa maana ya kuapload kwenye sehemu ya “local file”.

Ukishafanya  hatua moja wapo nilizozitaja hapo juu utatakiwa kubonyeza  sehemu ya kuwasilisha “submit” na kuona majibu husika.

Katika hatua hii utaweza kuona vipande vyote vya picha vilivyo tumika katika video hiyo na ukikibonyeza kipande chochote kati ya hivyo itakupeleka katika taarifa husika hivyo utaweza kufahamu habari hiyo imechapishwa lini, wapi na nani na utaweza kujua hata imechapishwa mara ngapi.

Kuthibitisha habari si miujiza hasa kipindi hiki cha teknolojia. Soma zaidi www.nukta.co.tz kwa maarifa zaidi.

Enable Notifications OK No thanks