Jeshi la Polisi: Hamza alikuwa gaidi

September 2, 2021 12:13 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Limesema alikuwa akijifunza vitendo hivyo kupitia mitandao ya kijamii.
  • Lasema hakuwa anamiliki fedha na madini kama inavyodaiwa.

Mwanza. Jeshi la Polisi limesema kuwa Hamza Mohammed, aliyeuawa wiki iliyopita baada ya kuwaua watu wanne kwa risasi, alikuwa gaidi wa kujitoa mhanga na alijifunza vitendo hivyo kupitia mitandao ya kijamii inayomilikiwa na makundi ya ugaidi duniani likiwemo la Al Shabab.

Hamza aliuawa Agosti 25, 2021 baada ya kutekeleza mauaji ya watu wanne, watatu kati yao wa polisi na mmoja wa kampuni binafsi ya ulinzi ya SGA kwa risasi jirani na balozi wa Ufaransa jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camillius Wambura amewaambia wanahabari leo (Septemba 2, 2021) jijini Mwanza kuwa katika uchunguzi waliofanya wamebaini kijana huyo alikuwa na viasharia vyote vya ugaidi kwa muda mrefu.

“Hamza Mohammed ni mtu ambaye alikuwa akiishi kisiri na mtu aliyegubikwa na viashiria vyote vya kigaidi kipindi cha kutosha. 

“Hamza Mohammed amekuwa akijifunza mambo mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii ambayo kwa kipindi kirefu amekuwa akijifunza mambo ya kigaidi kupitia mitandao inayoonyesha matendo ya Al Shabab na matendo ya vikundi kama ISIS yanayoendelea na magaidi wengi hujifunza kupitia mitandaoni,” amesema Wambura.

                     

Amesema uchunguzi wao ulijikita katika mambo makuu matatu: kutaka kutambua Hamza Mohammed ni nani, nini kilimsukuma kwenda kufanya tukio lile na kutaka kutambua mshiriki mwingine katika tukio hilo.

“Tabia zake na matendo yake kwa kipindi kirefu ameyapata kupitia mawasiliano na watu wengine wa baadhi ya nchi ambazo zina matendo kama hayo lakini kikubwa ni ugaidi kupitia mitandao yaani radicalisation (misimamo mikali) kupitia social media (mitandao ya kijamii),” amesema Wambura.

Amesema katika kuthibitisha kuwa Hamza alikuwa gaidi kutokana video zilizosambaa mtandaoni alikuwa anashambulia gari la polisi bila uwoga na hiyo ni kudhihirisha kuwa alikuwa haogopi na nia yake ni kuua askari.

Hata hivyo, amekanusha madai kuwa aliwashambulia askari hao kwa sababu walimdhulumu madini yake ambapo amesema katika uchunguzi wao wamebaini kuwa kijana huyo hakuwa na madini wala fedha.

“..watu wengi wameongea kwamba alikuwa anamiliki migodi ya madini kule Chunya na maeneo ya Makongolosi uchunguzi wetu umebaini hali hiyo ya maisha ilikwisha simama muda mrefu,” amebainisha  Wambura.

Aidha,  Polisi wamebaini kuwa Hamza alikuwa ni aina ya magaidi wanaoamua kuifia dini.

Wambura amewahakikishia wananchi kuwa Jeshi la Polisi limejitoa mhanga kuhakikisha linalinda raia na mali zake ili iwe salama kama walivyofanya kwenye tukio la Hamza.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
4 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
4 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴 LIVE: WABUNGE WAKIMCHAPA MASWALI MAZITO WAZIRI MKUU BUNGENI

🔴 LIVE: WABUNGE WAKIMCHAPA MASWALI MAZITO WAZIRI MKUU BUNGENI

Nukta TV

TANTRADE: Tumieni vifungashio vya "Made in Tanzania"

TANTRADE: Tumieni vifungashio vya "Made in Tanzania"

Nukta TV

Nukta Africa ndani ya Africa Agri Expo 2026

Nukta Africa ndani ya Africa Agri Expo 2026

Nukta TV