‘Janga jipya la mdudu anayeua India, China’ ni uzushi
- Kuna video zinazosambaa mtandaoni zikionyesha watu wanadondoka na kufariki kwa madai ya kuumwa na wadudu hao.
- Video hizo ni tukio la kuvuja kwa gesi katika mjini wa Visakhapatnam nchini India Mei 7, 2020.
Dar es Salaam.Zipo habari za uzushi zinazagaa mtandaoni zikisema kuwa kuna mlipuko wa ugonjwa mpya katika nchi za China na India ikiwa ni miezi kadhaa baada ya kutokea ugonjwa wa Corona (COVID-19) .
Habari hizo ambazo ziko katika mfumo wa video na picha ambazo zinasambazwa hasa katika mtandao wa WhatsApp hazina ukweli wowote kuhusu ugonjwa mpya katika nchini hizo.
Sehemu ya ujumbe huo inaeleza kuwa “ndugu zangu ktk imani inasemekana had saiv kuna balaa jengine limejitokeza huko China na India… Balaa wenyewe kuna mdudu mfano wake km nyuki akikutafuna tu kifo kina kutembelea haraka kuliko sumu ya nyoka…”
Ujumbe unaozagaa kwenye mitandao ya kijamii ukeleza kuzuka kwa balaa lingine huko China na India.PichaIMtandao
Ujumbe huo uliambatana na picha za video zaidi ya moja zizonaonyesha watu wakiwa wanaanguka na wengine wakiwa dhaifu sana huku wakibebwa kuingizwa kwenye magari binafsi na ya wagonjwa.
Je ukweli ukoje juu ya taarifa hizo
Uchunguzi wa Nukta Fakti ulifanywa kwa kutumia zana za kijigitali umebaini kuwa picha hizo na video zinazosambaa ni tukio la kulipuka kwa kinu cha gesi huko Visakhapatnam nchini India Mei 7,2020 lililoripotiwa na vyombo habari duniani.
Video hizo zinazogaa hazina uhusiano na ugonjwa huo unaosemekana unasababishwa na kun’gatwa na mdudu kama nyuki na kufanya watu kuwa wadhaifu bali watu hao wanaonekana ni wadhaifu kutokana na kuvuta hewa iliyochanganyika na gesi. Katika tukio hilo watu 12 walifariki dunia.
Pia picha ya mdudu inayosambaa (murder hornet) anayefanana na nyuki ambaye anadaiwa kuwa ana sumu kali kama nyoka sio kweli.
Wataalmu wa viumbe wamesema mdudu huyo ana madhara kwa binadamu lakini siyo kwa kiasi kikubwa.
Picha ya mdudu anaiyeitwa murder hornet Picha na mtandao.PichaIMtandao
Uamuzi wa mwisho
Habari hiyo inayodai kuibuka ugonjwa mpya katika nchi za China na India ni ya uongo au uzushi.
Endelea kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya ugonjwa wa virusi vya Corona kwa kunawa mara kwa mara na maji tiririka na sabuni, vaa barakoa kila utokapo nje, jizuie safari zisizokuwa na sababu
Latest