Instagram yafanya majaribio ya kuficha idadi ya “likes” na “views” za watumiaji wake

July 18, 2019 1:51 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Lengo la majaribio hayo ni kuwawezesha wafuasi wa akaunti za Instagram kuweka mawazo yao kwenye picha na video na siyo idadi ya likes au views alizopata mtu.
  • Yasema imezingatia maslahi mapana ya watumiaji wake.

Mtandao wa instagram unafanya majaribio katika nchi saba duniani ili kuzuia watu kuona idadi ya watu waliopenda (likes) na waliotazama (Views) picha na video ambazo zinawekwa kwenye mtandao huo. 

Lengo la majaribio hayo ni kuwawezesha wafuasi wa akaunti za Instagram kuweka mawazo yao kwenye picha na video na siyo idadi ya likes au views alizopata mtu. 

Majaribio hayo yanafanyika katika nchi za Australia, Brazil, Canada, Ireland, italia, Japan na New Zealand ambapo mtandao huo utaficha ‘likes’ na ‘views’ ambazo zimekuwa zikionekana chini ya video au picha iliyowekwa Instagram. 

Hata hivyo, mtu aliyeweka video au picha ataendelea kuona idadi ya watu walio like au kuangalia video yake. 

Majaribio hayo ambayo sasa yamenza kufanyika nchini Canada ambapo watu wanao like picha au kuangalia video katika mtandao huo wenye watumiaji zaidi ya bilioni 1.2 sasa hawataweza kuziona badala yake  wataona picha, video na ujumbe uliowekwa.


ZinazohusianaInstagram yaja na mbinu mpya kudhibiti uzalilishaji mtandaoni


Mkuu wa Instagram, Adam Mosseri katika mahojiano yake ya hivi karibuni na shirika la habari la  CBS News  amesema wamefanya majaribio hayo kwa ajili ya maslahi mapana ya watumiaji wake. 

“Hatutaki Instagram iwe na ushindani. Tunaka Iwe sehemu ambayo watu watatumia nguvu zao kwa ajili ya kujuana na watu wawapendao na vitu wanavyovijali zaidi,’’ amesema Mosseri

Mosseri amesema likes na views zitaendelea kuonekana kwa mtumiaji mmoja mmoja katika kipindi hicho cha majaribio lakini hazitaweza kuwekwa wazi kwa watumiaji wengine wa mtandao huo ili kupunguza misuguano na mitazamo hasi inayoweza kusababisha madhara.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanya na Taasisi ya RSPH (Royal Society for Public Health) mwaka 2017 unaeleza kuwa  mtandao huo ni hatari zaidi kwa afya ya akili kwa sababu unachangia kupata msongo wa mawazo na mkazoi (depression) na wasiwasi (anxiety).

Wanaoathirika zaidi ni vijana wanaotumia kwa muda mrefu mtandao huo.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
26 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
26 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV