Idadi ya waliofariki Katesh yafika 63

December 4, 2023 3:36 pm · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Wanawake wafikia 40 na wanaume 23.
  • Kati yao 23 ni watoto nchini ya miaka 18.

Dar es Salaam. Idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua za El Nino Katesh mkoani Manyara imefikia 63 huku zaidi ya nusu wakiwa ni wanawake na watoto.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliyekuwa akizungumza wakati wa kuaga miili ya marehemu hao  leo Novemba 4, 2023 amesema wanaume waliofariki kutokana na ajali hiyo wamefikia 23 huku wanawake wakiwa 40.

“Tumepoteza ndugu zetu 63, wanaume 23 na wanawake ni 40. Kati ya hawa, watu wazima kuanzia miaka 18 kwenda juu, wanaume ni 14 na wanawake ni 26, wanafanya ile jumla ya watu wazima 40 na watoto wadogo chini ya miaka 18, wanaume tisa na wanawake 14, wanafanya jumla ya 23.” amesema Waziri Mkuu.

Vifo hivyo ni vya wakazi wa mji wa Katesh hususan vijiji vya Jorodom, Ganana, Katesh na Dumbeta na vijiji vya Gendabi, Sarijandu, Arukushay, na Sebasi vinavyotajwa kuathirika zaidi.


Soma zaidi:Rais Samia kurejea nchini kufuatia zaidi ya vifo 50, Katesh


Majeruhi wafikia 116

Waakti idadi ya vifo ikiongezeka Idadi ya majeruhi imefikia 116, wanaume wakiwa 56 na wanawake 60 ambapo  kati yao watu wazima  60 na watoto chini ya umri wa miaka 18 wakiwa 66.

Aidha, Waziri Majaliwa ameeelza kuwa  mbali na mafuriko hayo kusababisha vifo vya watu na majeruhi pia  yamesababisha uharibifu mkubwa katika nyumba za kuishi migodi na ekari 750 za mashamba zikikadiriwa kuharibika.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiaga miili ya watu waliofariki kutokana na mvua za El Nino Katesh mkoani Manyara.Picha| Ofisi ya Waziri Mkuu.

Rais Samia atoa maagizo

Waziri Majaiwa amesema kutokana na maafa hayo Rais Samia ametoa maagizo mbalimbali kwa Wizara na mashirika ya Serikali ikiwemo kufanya tahmini ya madhara ya mafuriko hayo pamoja na kutoa huduma za malazi na chakula bure kwa wahanga.

Pia kiongozi huyo wanchi ameridhia Serikali yake kugharamia matibabu bure kwa majeruhi waliopo hospitaalini huku wale waliopoteza maisha wakihifadhiwa kwenye majeneza na kusafirishwa hadi katika failia zao kwa gharama za Serikali.

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mikakati ya Serikali kuhakikisha walimu wa VETA wanapata ajira na mikopo

Mikakati ya Serikali kuhakikisha walimu wa VETA wanapata ajira na mikopo

Nukta TV

Mama Salama alivyombana Wanu kuhusu maslahi ya walimu wanaojitolea

Mama Salama alivyombana Wanu kuhusu maslahi ya walimu wanaojitolea

Nukta TV

Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Kwanini uchafuzi wa mazingira ni tishio kwa afya ya binadamu na uchumi

Nukta TV