Hujuma zatajwa kuteketea mgahawa wa The Cask and Grill Mwanza

October 27, 2021 12:15 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Uliteketea kwa moto usiku wa kuamkia Oktoba 25.
  • Uchunguzi wabaini ajali hiyo imesababishwa na hujuma.
  • Ni mgahawa maarufu ka burudani mkoani Mwanza.

Mwanza. Jeshi la  Zimamoto na Uokoaji mkoani Mwanza limesema uchunguzi wa awali wa kuteketea kwa mgahawa maarufu wa The Cask Bar and Grill ni matokeo ya vitendo vya hujuma.

Mgahawa huo iliteketea kwa moto usiku wa kuamkia jumatatu Oktoba 25, 2021 majira ya saa 5 usiku wakati wateja wakiendelea kupata burudani ya muziki na vinywaji.

Kamanda wa Polisi wa Jeshi hilo mkoani Mwanza, Ambwene Mwakibete akizungumza na waandishi wa habari  jijini Mwanza leo Oktoba 27, amesema baada ya uchunguzi wa siku mbili wamebaini kwamba ajali hiyo ilitokana na hujuma.

Hata hivyo, Mwakibete hakusema ni hujuma gani, lakini amesema bado uchunguzi unaendelea ambao unahusisha  vyombo vingine vya  usalama.

“Tumebaini kulikuwa na vitendo vya hujuma, lakin pia niwaombe wananchi kuondoa dhana potofu iliyojengeka kwa jamii kwambaJeshi la  Zimamoto na Uokoaji linakwenda katika matukio ya moto huku magari yao yakiwa hayana maji,”  amesema  Mwakibete.

Hata hivyo, vyombo vya dola vinaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu ajali hiyo.

Awali  mmiliki wa mgahawa huo uliopo jengo la Rock City Mall, Joel Makanyaga alieleza kuwa hajui chanzo cha ajali hiyo hivyo wanahitaji muda wa kutafakari na kutambua nini kimetokea .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza,  Ramadhani Ng’anzi akizungumza alipotembelea eneo la tukio alisema ajali hiyo ilitokea wakati watu wakiendelea kuburudika na vinywaji.

Alisema moto huo ulianza kuwaka eneo la juu ya mgahawa huo na baadaye ulisambaa na kushuka chini na kuteketeza jengo lote.

“Baada ya kuona moto wafanyakazi walitoa taarifa polisi na sisi tuliwasiliana na zimamoto na kwa haraka walifika kuudhibiti moto huu ukizingatia jengo hili asilimia kubwa limejengwa kwa miti pamoja na mbao na kuwezekwa kwa bati hivyo moto ulikuwa unasambaa kwa kasi, lakini wameweza kuudhibiti ili usiweze kuenea katika majengo mengine,”  alieleza Ng’anzi.

Hata hivyo, mpaka sasa haijajulikana moto huo umesababisha hasara kiasi gani.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
14 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV