Hizi ndizo kompyuta bora kwa mwaka 2020

June 1, 2020 12:30 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Baba lao ambayo inafaa kwa takribani matumizi yote ni Dell XPS 13 ya mwaka 2020.
  • Kama wewe ni mpenzi wa michezo ya kompyuta unaweza kuangazia Asus Rog Zephyrus G14.
  • Kama hofu yako ni usalama wa taarifa zako, HP Elite Dragonfly ni mwisho wa reli.

Dar es Salaam. Hakuna furaha kwa mtu yeyote anayetumia kompyuta mpakato (laptop) kama kutumia kompyuta inayofanya kazi bila kusitasita. 

Iwe ni kazi ya kuhariri picha, kuandika ripoti, kusoma mtandaoni na mengineyo, utahitaji kompyuta ambayo haitakuangusha, yenye muonekano mzuri na inayokurahisishia kazi zako. 

Yote hayo huwezeshwa na uchaguzi wa kompyuta  wakati wa kununua ikiwemo kuzingatia uwezo wake wa kutunza kumbukumbu, muonekano, skrini, nguvu ya betri na mengine ili kuendana na shughuli unazozifanya.

Kama bado unawaza kununua kompyuta inayokidhi mahitaji yako, tovuti ya teknolojia ya The Verge imetoa orodha ya kompyuta ambazo ni bora kwa mwaka 2020. Je, ni zipi hizo kwanini zimechaguliwa kompyuta tano tu? 

05. HP Elite Dragonfly

Kompyuta hii imekuja na mifumo madhubuti kwa ajili ya usalama wa mtumiaji ikiiwemo kukupa nafasi ya kuzuia watu walio karibu yako kuangalia unachokifanya hasa ukiwa katika mikusanyiko.

Pia, kompyuta hiyo imetengenezwa na teknolojia ya “Tile Tracker” ambayo itakuwezesha kuwasha mlio (Alarm) yake pindi utakapoipoteza ila tu iwe kwenye anuai inayoweza kuunganishwa na “Bluetooth”.

Unaweza kuifuatilia kwa kutumia simu kokote itakapo kuwa duniani hata kama imezimwa. 

Sambamba na hilo ina kichapio chake (Keyboard) chenye betri linalotunza umeme kwa saa 11. 

Ili kuipata kompyuta hii itakuwabidi ikutoke Sh 4.4 milioni kwa bei ya leo (Juni1, 2020) yenye hadi jigabaiti 8 (GB8) za uhifadhi wa ndani (RAM) na GB 128 za uhifadhi wa kawaida ambayo unaweza kuongeza hadi telabaiti 2 (uwezo wa uhifadhi wa kuhifadhi vitu).

Unaweza kuifuatilia kwa kutumia simu kokote itakapo kuwa duniani hata kama imezimwa. Picha| Laptop Mag.

04. Macbook Pro (Inchi-16 2019)

Kwa mujibu wa The Verge, hili ni chagua zuri kwa wadau wanaohitaji kompyuta yenye nguvu kutoka kompyuta za Mac. 

Mbali na ukubwa wake wa inchi-16, kompyuta hii ni yenye sauti kuliko yeyote utakayoikuta sokoni. 

Kampuni ya Apple ambaye ni mzalishaji wa kompyuta hizi, imeweka spika tatu kwa kila upande wa komyuta hii huku kati yake mbili ni spika zenye kuhimili mdundo wa sauti ya chini yaani “Woofer”.

Kompyuta hii ina uhifadhi wa hadi TB1 , Turbo boost hadi 4.8GHz (teknolojia ya kuipa nguvu kompyuta inapoelemewa), na uhifadhi wa ndani (RAM) ya GB16 ambavyo hivyo vinakuja kwa gharama ya takribani Sh6.5 milioni.

Uko tayari kununua kompyuta ya Sh6.5 milioni? Kazi kwako. 

03. Asus Rog Zephyrus G14

Kwa wapenzi wa michezo ya kompyuta, hapa ndipo mahala pake. Kompyuta hii inaweza kuratibu michezo yenye uhitaji wa nguvu kubwa bila tatizo. 

Uwezo wa mfumo wake endeshi (CPU) yake ya “Nvidia RTX 2060 Max-Q” na ukubwa wa skrini yake wa  “HZ120”, utamuacha kila achezaye michezo ya kompyuta akiteleza tu.

Hata hivyo, siyo kwa wacheza michezo tu, hata wafanyabiashara wanaohitaji teknolojia hiyo wanaweza kufurahia kompyuta hii kwani ina muundo mzuri. 

Endapo utahitaji kufanya mikutano ya mtandaoni, kompyuta hii haitokufaa kwani haina kamera licha ya kugharimu takribani Sh3,4 milioni ikiwa na uhifadhi wa ndani wa GB16 na uhifadhi wa kawaida wa TB moja.

Endapo utahitaji kufanya mikutano ya mtandaoni, kompyuta hii haitokufaa kwani haina kamera. Picha| Neowin.

02. Macbook Air 2020

Kompyuta nyingine kutoka kampuni ya Apple ambayo inakuja na uzao (generation) wa 10 wa teknolojia ya “Intel Processors”. 

Komyuta hii pia ina teknolojia ya kuskani alama za vidole kwa ajili ya manunuzi na kuifungua. 

Hata hivyo, changamoto ya kompyuta hii ni kuwa haifai kwa matumizi makubwa kwa sababu utaishia kupata mwendo wa kobe kwenye utendaji kazi na feni yake inatoa sauti kubwa.


Zinazohusiana


01.  Dell XPS 13 (2020)

The Verge imesema hii ndiyo kompyuta nzuri zaidi unayoweza kununua kwa sasa kama pesa kwako siyo tatizo. 

Kama unahitaji komyuta ambayo inafanya takribani kila kitu kwa ufasaha ni Dell XPS 13 ya mwaka 2020 kwani ina kasi ya kuchakata vitu wakati wa kuitumia. 

Muonekano wa skrini yake ni kitu cha kwanza kinachoweza kuvutia macho yako kwani kioo kinachukua asilimia 91.5 ya sehemu yote ya skrini huku zilizosalia zikiwa ni sehemu zenye plastiki za kuishikilia skrini yake.

Mwanga wake wa nits (kipimo cha mwanga) 500 unatosha kwa yeyote mwenye kufanyia kazi ndani na hata nje.

Betri yake inayodumu kwa msaa saba, inafaa wote wanaotumia teknolojia hii wakiwa kwenye shughuli  zilizo mbali na umeme.  Kompyuta hii inabebeka kirahisi ikiwa na uzito wa kilo 1.21 

Uhifadhi wake wa kawaida unaenda hadi TB1 huku wa ndani ukiwa ni GB4, 8 na 16.

Hata hivyo, haya ni mapendekezo ya wadau wa teknolojia. Kuna kompyuta nyingi madukani zinazoweza kukufaa kwa kila kazi unayoifanya kulingana na mahitaji yako.

Enable Notifications OK No thanks