HESLB yaanika kozi zitakazopewa kipaumbele mikopo elimu ya juu 2022-23

July 15, 2022 11:54 am · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na ualimu wa sayansi.
  • Shahada ya lugha ya kiswahili yapewa kipaumbele kwa mara ya kwanza. 
  • Dirisha kufunguliwa Julai 19 mpaka Septemba 30, 2022.

Dar es salaam. Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa mwongozo wa utoaji mikopo kwa mwaka 2022/23 huku ikiweka wazi makundi matatu ya kozi zitakazopewa kipaumbele katika utoaji wa mikopo hiyo ikiwemo lugha ya Kiswahili.

Wakati HESLB ikitoa mwongozo huo, tayari Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imefungua dirisha la maombi ya udahili kwa waombaji wa shahada ya kwanza ambapo lipo wazi kuanzia Julai 8 hadi Agosti 5, 2022.

Dirisha la maombi ya mikopo la HESLB litakuwa wazi kwa muda wa siku 70 kuanzia Julai 19 hadi Septemba 30 mwaka huu ili kuwapa nafasi waombaji kupitia muongozo na kujaza taarifa zinazohitajika kwa ufasaha ikiwemo kuchagua kozi wanazotaka kusoma.

Kozi zilizopewa kipaumbele

Kundi la kwanza kwa mujibu wa HESLB, linahusisha kozi za ualimu wa Sayansi (fizikia, kemia na biolojia), ualimu wa hisabati na teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama).

Kozi nyingine ni za sayansi za afya ikiwemo udaktari,upasuaji meno,madawa ya mifugo,ufamasia,uuguzi,ukunga, shahada ya sayansi katika prosthetikia na mifupa, shahada ya sayansi katika mazoezi ya viungo, shahada ya sayansi ya afya na maabara,shahada ya sayansi yamaabara na matibabu na shahada ya sayansi ya teknolojia ya mionzi.

“Programu za uhandisi (ujenzi, mitambo, umeme, uchimbaji madini, utengenezaji nguo, kemikali na usindikaji, kilimo, chakula na usindikaji, magari, viwanda, usari majini, teknolojia ya uhandisi wa baharini, elektronikia na mawasiliano, usindikaji na huduma baada ya mavuno, maji na umwagiliaji, na uhandisi wa ndege,” heslb imeeleza katika mwongozo huo. 

Katika kundi hilo hilo la kwanza kuna programu nyingine kama jiolojia ya petroli, kemia ya petroli, mafuta na gesi, kompyuta, programu za sayansi ya kompyuta, habari na mitandao, takwimu bima (actuarial and data sciences), kilimo, misitu, sayansi ya wanyama na uzalishaji pamoja na shahada ya awali ya sanaa katika kiswahili imeongezeka kwa mara ya kwanza..

Kundi la pili 

Kundi la pili ambalo litapewa kipaumbele katika dirisha la maombi ya mikopo mwaka 2022/23 ni programu za msingi za sayansi inayohusisha shahada ya sayansi kwa ujumla katika wanyama, mimea, kemia, fizikia, baiolojia, baiolojia ya viumbe vidogo, baiolojia ya mifugo na bioteknolojia.

“Uvuvi na mifugo, sayansi ya mazingira na uhifadhi, matibabu, hisabati na takwimu, sayansi ya mazingira na usimamizi, afya na mazingira, baioteknolojia na maabara, wanyamapori na uhifadhi, kompyuta na tehama, vipimo na mizani, mazingira na maendeleo ya miji,” inasomeka sehemu ya mwongozo kuhusu kozi za kundi la pili.

Pia watakaosoma programu ya sayansi ya ardhi ikiwa ni pamoja na ubunifu majengo, ubunifu mandhari nje ya majengo, usanifu ndani ya majengo, uchumi ujenzi, mipango miji na vijiji,usimamizi na uthaminishi ardhi,j iospasho pamoja na teknolojia katika usanifu.


Soma zaidi: 


Kundi la tatu ni hili.

Kwa wale wale watakakaosoma masomo ya biashara na uongozi, sayansi za jamii, uhasibu, masoko, fedha, uchumi, takwimu, mazingira, maendeleo ya jamii, ustawi wa jamii, masomo ya maendeleo, sosholojia, sayansi ya siasa, sanaa, uchoraji, sayansi ya ubunifu wapo katika kundi la tatu. 

Aidha masomo ya  muziki, sheria, lugha, fasihi, jiograa, saikolojia, anthropolojia, akiolojia na masomo ya uandishi wa habari na mawasiliano pamoja na programu nyingine zote ambazo hazijaorodheshwa katika kundi lolote kati ya hayo matatu, zitaangukia katika kundi hili  la tatu.

Kwa mujibu wa mwongozo huo uliochapishwa katika tovuti ya heslb julai 12, 2022 umebainisha kuwa ada ya kuainisha waombaji, wahitaji, na kuonyesha taratibu zinazotakiwa  makundi ya programu  zenye vipaumbele zitapewa mikopo kulingana na uwepo wa fedha.

Bodi ya mikopo imesema mikopo hiyo itakayotolewa kwa wanafunzi wa elimu ya juu itajumuisha gharama za chakula na malazi, da ya mafunzo, vitabu na viandikwa, ahitaji maalumu ya kitivo, utafiti na mafunzo kwa vitendo.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW