Haya ndiyo maajabu ya ‘sabufa’ ya LG itakayoingia soko 2022

December 20, 2021 9:02 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Ina spika zenye uwezo wa kusafirisha sauti kwa mwelekeo wa juu (wima).
  • Ni spika za kwanza zenye uwezo huo kuwahi kutengenezwa na LG.
  • Bei ya sokoni bado sintofahamu.

Dar es Salaam. Spika nyingi zilizopo sokoni zimebuniwa kupeleka mawimbi ya sauti kwa mwelekeo wa mbele au pembeni.

Hiyo inamaanisha, mawimbi wa sauti yanasafiri kwa mwelekeo wa mlalo (horizontal) pekee.

Kampuni ya kutengeneza vifaa vya kielektroniki ya nchini Korea Kusini  yaLG inatarajia kuingiza sokoni mfumo wa sauti (sound system) ambao mtumiaji wake atakuwa na uwezo wa kusikia muziki au chochote anachosikilizia kwenye sabufa kwa mwelekeo wa wima (vertical).

Haimaanishi ya kuwa spika zingine za mfumo wa mlalo zimetelekezwa, hapana! Ni kuwa spika hizo zitakuja zikiwa zimekamilika katika mifumo yote ukiwemo huo mpya.

Hii ni mara ya kwanza kwa LG  kutoka na teknolojia hiyo kati ya bidhaa zote za muziki iliwahi kuingiza sokoni.

LG imesema spika hiyo inafanya kazi kwa kupeleka mawimbi ya sauti juu ambapo yatadunda kwenye dari na kurudi kwenye chumba. 

Hiyo itaongeza ufanisi wa sauti kwa msikilizaji na hata uwezo wa kusikiliza sauti za mfumo wa nyuzi 360.

Muonekano wa jinsi LG S95QR inasafirisha mawimbi ya sauti. Picha| The Verge.

Kunani sauti za wima?

Kampuni hiyo imeipatia bidhaa hiyo jina la LG S95QR na lengo kuu la toleo hilo ni kumuongezea mtu furaha pale anapotumia spika hizo kutazamia filamu, kusikilizia muziki na hata kucheza michezo ya video.

Kama umewahi kutembelea kumbi za kuangalizia filamu, kuna muda unasikia sauti ya ndege inatokea juu hasa pale filamu inapomweka fanani kwenye mazingira ya msituni. Sauti inakuwa kama inakuvuta kwenye uhalisia fulani hivi.

Kwa  LG S95QR, inampatia mtumiaji uwezo wa kusikiliza sauti katika mwelekeo wa sehemu tatu yaani 3D.

Seti ya LG S95QR inakuja na spika nne. Spika kuu, spika mbili ndogo na spika ndefu (sound bar) ambazo zote zinafanya kazi kwa mfumo wa bila waya.


Soma zaidi:


Sokoni lini ?

Kwa mujibu wa LG, spika hizi zitaanza kuonyeshwa kwa wadau kuanzia Januari 4, 2022 ambapo watu wataziona kupitia hafla ya mtandaoni ya CES booth.

Hadi sasa LG haijatoa taarifa za bei yake au lini LG S95QR zitaingia sokoni tayari kwa watu kununua.

Hapa LG imekwama

Licha ya ngonjera nyingi ambayo LG imeimba kuhusu bidhaa yake, bado wadau wa teknolojia wameona baadhi ya mapungufu.

Shirika la habari la The Verge limesema baadhi ya vitu vinaweza visifanya kazi na teknolojia hii hasa kwa wapenzi wa michezo ya video ikiwemo PS5.

Follow Us on TikTok

FOLLOW NOW

Subscribe to Our YouTube Channel

SUBSCRIBE NOW