Hatua zinazoweza kumrejesha Dk Nchimbi CCM

August 27, 2026 6:12 pm · Emmanuel Tungaraza
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni pamoja na kukata rufaa na kuomba upya uanachama ikiwa atarejea CCM.
  • Mwenyekiti wa UVCCM, Mohamed Kawaida ameiambia Nukta Habari kuwa Dk Nchimbi anaweza kurejea CCM ikiwa ataiomba msamaha NEC.

Dar es Salaam. Kufukuzwa uanachama ni miongoni mwa hatua kali za kinidhamu ambazo chama cha siasa kinaweza kuchukua dhidi ya mwanachama anayekiuka katiba, kanuni au taratibu za chama.

Jana, Agosti 26, 2026 Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ilitangaza kumfukuza uanachama Dk Emmanuel Nchimbi siku moja baada ya kutangaza kuwa angejiuzulu ifikapo Septemba 4 mwaka huu.

Katibu Mkuu wa CCM, Dk Asha Rose-Migiro aliwaambia wanahabari usiku wa jana kuwa uamuzi huo umetokana na ukiukwajii mkubwa wa maadili wa Dk Nchimbi akimtaja Deogratius Ndejembi kuwa mrithi wake kabla ya kupitishwa na Bunge la Tanzania.

Kwa karibu saa 10 zilizopita tangu kutolewa kwa uamuzi huo, swali linalobakia ni nini kinafuata baada ya Dk kufutwa uanachama, je anaweza kurejea katika siasa za chama hicho kikongwe zaidi Tanzania?.

Anaweza kukata rufaa

Kufukuzwa uanachama hakumaanishi kuwa Dk Emmanuel Nchimbi hana njia ya kupinga uamuzi huo. Kwa mujibu wa Ibara ya 13(3) ya Katiba ya CCM ya mwaka 1977, Toleo la Desemba 2022, mwanachama aliyeadhibiwa kwa kufukuzwa ana haki ya kukata rufaa au kujitetea dhidi ya uamuzi huo.

Hivyo, hatua ya kwanza ambayo Dk Nchimbi anaweza kuchukua ni kutumia utaratibu wa rufaa uliowekwa ndani ya chama ili kupinga uamuzi wa kumfukuza uanachama.

Katika hatua hiyo, anaweza kuwasilisha hoja zake za utetezi na kueleza sababu za kutoridhishwa na uamuzi uliochukuliwa dhidi yake.

Iwapo Dk Nchimbi atashinda rufaa na uamuzi wa kumfukuza uanachama ukabatilishwa, ataendelea kuwa mwanachama wa CCM.

Iwapo rufaa yake haitafanikiwa na uamuzi wa kufukuzwa ukabaki, akitaka kurejea CCM atalazimika kuomba upya uanachama kwa kufuata utaratibu kama ilivyoainishwa katika ibara ya 13(3) ya katiba ya chama hicho.

“Mwanachama aliyeachishwa au kufukuzwa uanachama akitaka kuingia tena katika CCM, itabidi aombe upya, na atapeleka maombi yake hayo ama katika Halmashauri Kuu ya Wilaya ama kikao kilichomwachisha au kumfukuza Uanachama,” imeeleza sehemu ya ibara hiyo.

Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Mohamed Ali Mohammed (Kawaida) ameiambia Nukta Habari kuwa Dk Nchimbi anaweza kurejea CCM ikiwa ataiomba msamaha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC).

“Anaweza kurudi kama Kina Membe (Bernard Membe), akiomba msamaha na NEC ikiridhia,” amesema Kawaida.

Anaweza kuibukia chama kingine

Mchambuzi wa mchambuzi wa masuala ya kisiasa, Ephron Mkungilwa anaeleza kuwa licha ya Dk Nchimbi kuruhusiwa kurejea CCM kikatiba, anaweza kuamua kuibukia katika vyama vingine vya kisiasa.

“Kurejea kwake itategemeana ni nani yupo ndani ya chama na ni nani anakiongoza chama, lakini itategemeana na mwelekeo wake kwa wakati huo, huenda akaibukia na kurejea katika siasa ndani ya chama kingine,” amesema Mkungilwa.

Mkungilwa pia amesema ikiwa kiongozi huyo ana faida, bado chama hicho kinaweza kumrudisha kama ilivyokuwa miaka ya nyuma alipowekwa kando kwa makosa ya kimaadili na baadae kurudishwa na kutumikia nafasi mbalimbali za uongozi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
27 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
27 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
27 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Dk Nchimbi afukuzwa CCM, Ndejembi akipendekezwa kuchukua mikoba

Dk Nchimbi afukuzwa CCM, Ndejembi akipendekezwa kuchukua mikoba

Nukta TV

Haya hapa mafao ya Dk Emmanuel Nchimbi aking’atuka madarakani

Haya hapa mafao ya Dk Emmanuel Nchimbi aking’atuka madarakani

Nukta TV

SIMULIZI: Namna Magufuli, Samia walivyoichonga historia ya Bwawa la Mwalimu Nyerere

SIMULIZI: Namna Magufuli, Samia walivyoichonga historia ya Bwawa la Mwalimu Nyerere

Nukta TV