Hatua rahisi za kufuta akaunti yako YouTube

October 3, 2022 12:46 pm · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni kwa kufuata maelezo yanayotolewa na mtandao huo.

Dar es Salaam. Endapo umechoshwa na mtandao wa YouTube ama unataka kuachana na matumizi ya akaunti unayoitumia kwa sasa, huu ni mwongozo wa haraka na rahisi unaokuonyesha jinsi ya kufuta kabisa akaunti na maudhui yake.

Mahitaji muhimu kukamilisha zoezi hili ni akaunti yako ya YouTube, kompyuta au simu janja, na kivinjari cha wavuti au programu ya YouTube ya simu.

Kulingana na mpangilio wako, unaweza kufuta chaneli yako ya YouTube, video, maoni na ujumbe lakini akaunti yako inaweza kubaki kwa sababu imeunganishwa na programu ya Google.

Jinsi ya kufuta chaneli yako ya YouTube 

Hatua ya 1: Ingia kwenye YouTube Studio ukitumia akaunti ya chaneli unayotaka kufuta. Chagua mpangilio kutoka upande wa kushoto wa skrini.



Hatua ya 2: Kwenye skrini inayofuata, chagua chaneli na kisha uchague kipengele cha mpangilio wa kina (advanced settings).

Hatua ya 3: Kwenye mpangilio wa kina, sogeza chini hadi uone chaguo la ondoa maudhui ya YouTube. Bofya chaguo hilo. Hii itafungua kipendele kingine, na utaombwa uingie katika akaunti yako tena.

Hatua ya 4: Bofya chaguo lililoandikwa “ninataka kufuta maudhui yangu kabisa.” Kuchagua chaguo hili kutalipanua katika maelezo mawili mafupi ya maana ya uamuzi huu, pamoja na visanduku vya kuteua karibu na kila sehemu ya maelezo. Soma maelezo haya, na ikiwa bado ungependa kufuta maudhui yako, chagua visanduku vya kuteua vyote viwili.

Hatua ya 5: Iwapo una uhakika wa kufuta chaneli yako ya YouTube, endelea na ubofye kitufe cha bluu kilichoandikwa “Futa maudhui yangu. 


Soma zaidi:

Hata kwenye simu inawezekana

Watumiaji wa simu za Android wanaweza kutumia maelekezo yafuatayo kufuta akaunti zao:

Hatua ya 1: Fungua programu ya YouTube kwenye kifaa chako. Chagua aikoni ya picha yako ya Wasifu kwenye kona ya juu kulia ya skrini yako. Chagua Dhibiti akaunti yako ya Google.

Hatua ya 2: Chagua Data na faragha.

Hatua ya 3: Sogeza chini hadi uone sehemu ya Pakua au ufute data yako. Katika sehemu hii, chagua futa huduma ya Google.

Hatua ya 4: Utaulizwa kuingia kwenye akaunti yako. Fanya hivyo. Baadaye, utapewa chaguo la kupakua data yako kabla ya kufuta chaneli yako ya YouTube. 

Hatua ya 5: Utaulizwa kuingia tena. Fanya hivyo. Kisha, gusa chaguo lenye lebo ninataka kufuta maudhui yangu kabisa. Kuchagua chaguo hili kutalipanua katika sehemu mbili za maelezo zinazoelezea uamuzi unao umaanisha.

Soma maelezo, kisha uchague visanduku vya kuteua vyote viwili ikiwa unaelewa na bado ungependa kufuta kituo chako cha YouTube.

Hatua ya 6: Ukiwa tayari kufuta chaneli yako, gusa kitufe cha bluu Futa maudhui yangu.


Tangazo

Jinsi ya kufuta chaneli yako ya YouTube kwenye iOS

Hatua ya 1: Kutoka skrini ya nyumbani, gusa aikoni ya Wasifu wako kwenye kona ya juu kulia na ubofye dhibiti akaunti yako ya Google.

Hatua ya 2: Bofya kwenye data na ubinafsishaji kutoka kipengele cha juu. Sogeza chini na ubofye Futa huduma au akaunti yako.

Hatua ya 3: Kuanzia hapo, unaweza kuamua kufuta huduma mahususi au akaunti yako ya Google kabisa. Ili kufuta chaneli yako, chagua futa huduma ya Google. Utaulizwa kuingiza nenosiri lako.

Hatua ya 4: Baada ya kuweka nenosiri lako, bonyeza aikoni ya Tupio karibu na YouTube, na data yako yote itaondolewa.

Baada ya kufuata hatua hizi kwa mtumiaji husika kulingana na kifaa chako, sasa unaweza kukamilisha zoezi la ufutaji wa akaunti yako ya YouTube.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV