Hapana: Uviko-19 haisambai kwa maji wala kuogelea

September 15, 2022 3:22 pm · admin
Share
Tweet
Copy Link
  • Wataalamu wa afya  wafafanua njia kuu ya kuambukiza ni kupitia hewa. 
  • Washauri watu kuendelea kuchukua tahadhari zinazotakiwa.

Wataalamu wa afya kutoka Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) wameeleza kwamba ugonjwa wa Uviko-19 hausambai kwa njia ya maji au watu kuogelea pamoja katika bwawa au chanzo chochote cha maji.

Ufafanuzi huo unatokana na kuendelea kuwepo kwa imani potofu juu ya namna homa ya Uviko-19 inavyosambaa na baadhi ya watu kuanza kuamini kuwa maji au kuogelea kunaweza kusababisha wapate homa hiyo.

Kumekuwa na tabia ya baadhi ya watu kuupuzia afua za kudhibiti ugonjwa huo ikiwemo kupata chanjo ya Uviko-19 nchini Tanzania licha ya ukweli kuwa ugonjwa huo umeendelea kuathiri watu wengi ulimwenguni ikiwemo kupoteza maisha yao. 

Hadi jana Septemba 14, 2022, WHO inaeleza watu milioni 600 wameripotiwa kuambukizwa Uviko-19 ulimwenguni kote huku watu milioni 6.4 wakipoteza maisha.

Hata hivyo, wataalamu wa afya wameonya kwamba kwa kuwa njia kuu ya kuambukizwa ugonjwa huo ni kupitia kubadilishana hewa na mtu mwenye maambukizi basi ni vema kukaa umbali wa mita moja, kuvaa barakoa na kuepuka mikusanyiko ya watu ili kuepuka ugonjwa huo.

​

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
18 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
18 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mambo ya kuzingatia unapoanzisha chombo cha habari mtandaoni (ONLINE MEDIA)

Mambo ya kuzingatia unapoanzisha chombo cha habari mtandaoni (ONLINE MEDIA)

Nukta TV

HELSB yatoa majina wanufaika wa mkopo awamu ya kwanza

HELSB yatoa majina wanufaika wa mkopo awamu ya kwanza

Nukta TV

TBS yatoa tahadhari matumizi ya ‘sponge’ kupika chapati

TBS yatoa tahadhari matumizi ya ‘sponge’ kupika chapati

Nukta TV