Sio kweli: Thabo Mbeki hajafariki dunia

January 3, 2024 2:50 pm · Daniel Mwingira
Share
Tweet
Copy Link

Dar es Salaam. Kumekuwa na taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii na  baadhi ya vyombo vya habari Tanzania kuwa, Rais mstaafu  wa awamu ya pili wa Afrika Kusini Thabo Mbeki  amefariki dunia lakini habari hiyo haina ukweli wowote.

Taarifa za kifo cha Mbeki zilianza kusambaa leo Januari 3, 2024 katika mitandao tofauti tofauti ikiwemo mtandao wa kijamii wa X sambamba na baadhi ya magazeti na radio za hapa Tanzania pamoja vyombo vya habari vikubwa  vya nje ya nchi

Ukweli ni huu

Nukta Fakti kupitia vyanzo mbalimbali vya habari vya ndani ya Afrika kusini na vingine vya kimataifa imethibtisha kuwa habari hiyo haina ukweli wowote.

Pia wakfu wa Thabo Mbeki (Thabo Mbeki Foundation) umetoa tarifa kupitia mtandao wa kijamii wa X (TMF foundation) ukieleza hali ya Afya ya Rais huyo mstaafu. 

Ukiwa na kichwa cha habari Statement Regarding President Thabo Mbeki’s Health katika tafsiri isiyo rasmi (Taarifa ya afya kuhusu Rais Thabo Mbeki) 

Katika taarifa hiyo kwa vyombo vya habari wamekanusha taarifa zinazosema Rais mstaafu Thabo Mbeki amefariki dunia kwa kuwa ni mzima wa afya.

Kwa hapa Tanzania gazeti la mwananchi lilikanusha habari hiyo kuwa haina ukweli wowote na kuomba radhi wasomaji wake kupitia chapisho kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
15 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Rais Samia: Kalamu yangu ina hatari, sijawahi kusaini mtu kunyongwa

Nukta TV

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Rais Samia: Matumizi jina Samia, likiwa kila mahali inachosha, tafuteni wengine

Nukta TV