Google yaingiza sokoni mtandao mpya wa kijamii

July 15, 2019 10:17 am · Daniel
Share
Tweet
Copy Link
  • Unajulikana kama Shoelace na umeanza kwa majaribio katika mji wa New York, Marekani. 
  • Umebuniwa takriban miezi mitatu tangu mtandao wa Google+ ifungwe. 
  • Unafanya kazi kwa watumiaji wa simu za Android and Apple wenye akaunti ya Google.

Kampuni ya teknolojia ya Google imeanzisha jukwaa jipya la mtandaoni lenye lengo la kuwaleta pamoja watu wenye mtazamo sawa kupitia matukio  mbalimbali au vitu wanavyovipenda.

Hatua hiyo imekuja Ikiwa ni miezi mitatu  tangu kampuni hiyo ya Marekani ilipotangaza kuufunga mtandao wake wa Google + Aprili mwaka huu.

Jukwaa hilo litakuwa linaendeshwa na rrogramu tumishi ya simu iliyopewa jina la Shoelace  ambapo itakuwa inafanya kazi ya  kumshauri mtu kila siku kuhusu tukio linalotokea karibu yake ikiwemo maonyesho ya bure au michezo mbalimbali  inayofanyika karibu na eneo analoishi.

Kwa sasa Shoelace inafanyiwa majaribio katika Jiji la New York na unapatikana kwa watu wachache kupitia kitengo cha Google kinachohusika na  majaribio cha Google Area 120.


Zinazohusiana: 


“Lengo kubwa la kuanzishwa kwa Shoelace ni kuwakutanisha watu pamoja hasa wale wenye malengo au vitu vinavyofanana,‘’ imesema sehemu ya taarifa ya Google  kwenye  tovuti ya  shoelace.

Lakini watakaohitaji mtandao huo kuwafikia katika maeneo yao wanatakiwa kuomba ‘code’ maalum ili kupata huduma hiyo.  

Programu tumishi hiyo inafanya kazi katika simu za Android kuanzaa kuanzia toleo la  v.8.0 na simu mpya ambapo watumiaji wa simu za Apple kuanzia toleo la  v.11.0 na mpya zaidi ya hapo. Kigezo kingine cha kutumia mtandao huo ni lazima uwe na akaunti ya Google. 

Hata hivyo, mtandao huo utaweza kushindana na kujipatia wafuasi wengi kama ilivyo kwa Facebook, Instagram na WhatsApp ambayo imetawala soko la mitandao ya kijamii duniani. 

Enable Notifications OK No thanks