Google yafungua fursa kwa wafanyabiashara 2020

January 16, 2020 9:26 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Imeingia ubia na programu tumishi ya Pointy kuwasaidia wafanyabiashara kupata soko kwa njia ya mtandao.
  • Sasa bidhaa na huduma kupatikana kwa urahisi katika sehemu ya kitafutio cha viti cha Google.
  • Huenda ikawasaidia wafanyabiashara kuongeza wigo wa soko na mapato.

Dar es Salaam. Wafanyabiashara wa Tanzania wenye mpango wa kuzipeleka biashara zao mtandaoni, sasa wana kila sababu ya kufurahi baada ya kampuni ya Google kuwafungulia fursa ya kutafuta soko la bidhaa na huduma zao kwa haraka na urahisi.

Kampuni hiyo ya Marekani imeingia ubia na programu tumishi ya Pointy ya Uingereza, inayomuwezesha mfanyabiashara kuweka bidhaa zake mtandaoni na kupewa kipaumbele katika  sehemu ya kutafutia cha vitu (browser) cha Google. 

Programu hiyo inarahisisha upatikanaji wa haraka wa bidhaa au huduma katika mtandao wa Google ambao umekuwa ukitumiwa na wafanyabiashara kujitangaza mtandaoni.


Zinazohusiana:


Ili kutumia fursa hiyo, mfanyabiashara anatakiwa kupakua programu tumishi ya Pointy, kisha kuweka bidhaa zake katika kipengele kinachoonyesha bidhaa mpya zilizopo sokoni kinachosimamiwa na Google, na kupata soko  la watu watakaokuwa wanaotafuta bidhaa hiyo kwenye Google.  

Pia itasaidia shughuli mbalimbali za kuendesha biashara zikiwemo utunzaji wa taarifa, ufanyaji wa mahesabu na tathmini ya mwenendo wa biashara kwa ujumla.

Hata hivyo, Google bado hawajabainisha siku rasmi mfumo huo utakapoanza kufanya kazi na taratibu wanazotakiwa kufuata wafanyabiashara ili kunadi bidhaa zao mtandaoni.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
16 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
16 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
16 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Magonjwa haya matano yanayoongoza kwa kuua watu duniani

Nukta TV

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Mambo yakuzingatia kabla ujawasha gari lako asubuhi

Nukta TV

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Kutana na ‘Poultry Plucker’, mashine inayonyonyoa kuku watatu kwa dakika moja

Nukta TV