Google Maps kuwaongezea ‘vibe’ jipya watumiaji wake

September 29, 2022 7:30 am · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Inaboresha programu yake kuwawezesha kufahamu shughuli zinazofanyika katika eneo husika.
  • Hii itasaidia watu kufanya maamuzi sahihi.

Dar es Salaam. Kama wewe ni mtumiaji wa programu ya Google Map kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo usafiri, basi utaongezewa ‘vibe’ lingine kukidhi mahitaji yako.

Programu hiyo inayoendeshwa na kampuni ya Google, imefanya maboresho na kuongeza kipengele kipya ambacho kinamuwezesha mtu kufahamu shughuli zinazofanyika katika eneo husika kabla hajafika.

Google imesema hatua hiyo itamsaidia mtu kufanya maamuzi ya kwenda au kutokwenda katika eneo husika kulingana na uchaguzi wake. 

Baadhi ya shughuli utakaziona katika programu hiyo ni pamoja na hali ya foleni, hali ya hewa na shughuli zinazoendelea katika eneo husika ikiwemo, biashara, migahawa, maduka na michezo. 

Shughuli hizo utazipata kwa picha na maelezo ambayo programu hiyo itakusogezea katika simu yako. 

“Tunafanya maendeleo mengine makubwa katika uchoraji wa ramani kwa kuleta maarifa muhimu – kama vile hali ya hewa na jinsi eneo lilivyo na shughuli nyingi maishani kwa mwonekano wa kina katika Ramani za Google,” ameeleza Prabhakar Raghavan, Makamu wa Rais Mwandamizi wa Search On.


Soma zaidi

Maboresho hayo mapya yanayokuja hivi karibuni yatakusaidia kulifahamu eneo kiundani kabla ya kuwasili, kuchunguza alama zaidi ya 250 katika mwonekano wa angani, sambamba na kutafuta maeneo ya karibu kwa taswira halisi.

“Tunafikiria upya Google Maps tena, tukiwa na ramani inayoonekana na angavu inayokuruhusu kufurahia eneo kana kwamba uko hapo,” amesema Chris Phillips Makamu na Meneja Mkuu, kitengo cha Google Geo.

Google imesema kwamba kipengele cha vibe kinakuja kwenye Ramani za Google kwenye simu zinazotumia mifumo endeshi ya iOS na Android katika miezi ijayo, lakini tarehe ya kipengele hicho kuanza kufanya kazi bado haijawekwa wazi.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
17 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Siku ya Familia, Mtoto wa Afrika kuadhimishwa Juni 30, 2026

Nukta TV

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Wadau wa 'kubet" watoa ya moyoni, pendekezo kupanda kwa tozo 5%

Nukta TV

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Wasemayo wananchi, vocha za kukwangua kupigwa maruku mijini

Nukta TV