Google, Expedia wazindua bidhaa mpya ya safari
- Wamezindua teknolojia itakayomwezesha msafiri kuratibu safari na mahali atakapofikia kwa njia rahisi ya kinasa sauti.
- Baadhi ya watu waifagilia wasema inawasaidia kufika popote duniani.
Kampuni za Google na Expedia wamerahisisha mchakato wa kusafiri kimataifa kwa ajili ya shughuli mbalimbali ikiwemo mapumziko ya mwisho wa mwaka.
Expedia Action, kampuni inayoratibu usafiri wa ndege ikishirikiana na moja ya bidhaa ya Google ya “Google Assistant” wamezindua teknolojia itakayomwezesha msafiri kuratibu safari na mahali atakapofikia kwa njia rahisi ya kinasa sauti.
Mtu anayetaka kutumia teknolojia hiyo anapaswa kufungua akaunti katika aprogramu tumishi ya Google Assistant kisha na ataunganishwa na mfumo wa expedia ili kupata urahisi anapotoa taarifa zake kabla hajaanza safari.
Programu hii inawafaa zaidi wale wanaosafiri nchi za nje ambazo hawana uzoefu nazo, kwani inamsaidia kupata usafiri wa uhakika na mahala pazuri pa kufikia ikiwemo hoteli inayoendana na mfuko wake.
Pia inampa mtu taarifa za kina za eneo analokwenda na kumshauri ni vitu gani anapaswa kubeba ili kuendana na mazingira mapya atakayofikia.
Zinazohusiana:
- Apps zinazoweza kukusaidia unapokuwa safarini
- Usafiri wa ndege unavyoweza kukutanisha na mwenza wa maisha
Nancy George mtalii kutoka Tanzania anayetarajia kusafiri hivi karibuni kuelekea Uingereza kwa mara ya kwanza ameiambia www.nukta.co.tz kuwa teknolijia hiyo itamrahisishia safari yake na kuifanya iwe ya mafanikio, kwa sababu teknolojia hiyo inatoa suluhisho kamili.
“Moja ya mambo yaliyokuwa yananitatiza ni mazingira nitakayoenda kukutana nayo, ambapo sitakua najua kitiu chochote,” amesema Nancy na kueleza kuwa baada ya kuifahamu teknolojia hiyo, sasa hana wasiwasi tena.
Teknolojia hiyo ni muendelezo wa wabunifu kubuni programu rahisi zinazoweza kuwawezesha wasafiri kwenda mahali popote bila kuhofia usalama wao, kwa sababu inawaongoza kwa kila kitu wanachofanya.