Filamu mpya tatu za kuangalia wiki hii

August 23, 2019 11:49 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Filamu hizo ni pamoja na “Angel has Fallen” yenye waigizaji nguli kama Morgan Freeman na Jada Pinkett Smith.
  • Zimejaa vifa vingi vya kusisimua vitakavyokupa funzo kubwa la maisha. 
  • Zitaonyeshwa kwa siku sita mfululizo kuanzia leo katika kumbi mbalimbali.

Dar es Salaam. Moja kati ya burudani ambazo hufurahisha watu wengi ni filamu. Kama wewe ni mmoja wa wapenzi wa starehe hiyo, basi upo kwenye ukurasa sahihi.

Hizi ndizo filamu mpya zitakazoonyeshwa kwenye kumbi za filamu kwa siku sita mfululizo kuanzia leo Agosti 23, 2019.

Angel has Fallen

Ikiwa imegharimu Dola za kimarekani milioni 80 (Sh183.9 bilioni), filamu hii inamhusu Mike Banning ambaye anashitakiwa baada ya kushindwa jaribio la kumuua Rais Tumbull. Baada ya kufanikiwa kuwatoroka waliomkamata, Banning analazimika kujificha ili FBI na mawakala wake wasimkamate. 

Baada ya kuujua ukweli kuhusu usalama wa Rais Tumbull, Banning atafanya nini kuhakikisha hakamatwi?

Mfuatilie Gerard Butler (Mike Banning) ambaye pia ameshiriki kwenye filamu zaidi ya 40 zikiwemo Gods of Egypy (2016) na Olympus has Fallen (2013) akiwa na waigizaji nguli kama Morgan Freeman na  Jada Pinkett Smith.

Usalama wa Rais Allan Trumbull upo kwenye maamuzi ya Mike Banning. Je itaweza?. Picha| Mtandao.

Tera Willy

Baada ya chombo chao cha kusafiria angani kuharibika wakiwa safarini, William anatenganishwa na wazazi wake. Sehemu ya chombo hicho ambamo yeye alikuwemo, inaangukia kwenye sayari isiyojulikana. 

Je kupitia msaada wa mbwa ambaye ni roboti atafanikiwa kuishi? Fuatilia kisa hiki cha kufikirika ambacho kina uhalisia wa nchi ya Ufaransa ambacho kimesimamiwa na Eric Tosi ambaye pia ameongoza a filamu za kufikirika zaidi ya nne ikiwemo ya Jungle Bunch (2017) na Spike (2012).


Zinazohusiana:


Ready or Not

Filamu hii ni komedi ya kutisha iliyosimamiwa na Matt Bettinelli-Olpin na Tyler Gillet ambayo inasimulia kisa cha kutisha kati ya wakwe na bibi harusi Samara Weaving. Baada ya kufunga ndoa, Weaving anafikiri kujikuta kwenye ukumbi mzuri kwa ajili ya tafrija ya harusi yake na mumewe Mark O’Brien lakini loo! Anajikuta kwenye ukumbi uliosheheni silaha ambazo zingine hajawahi kuziona.

Fuatilia kuona jinsi mapanga, shoka na hata mishale inavyotumika kumuwinda mkwe mpya wa familia ya O’Brien.

Ikiwa imegharimu Dola za Marekani milioni sita sawa na takribani Sh13.7 bilioni, Ready or Not ilizinduliwa kwa mara ya kwanza kwenye maonyesho ya kimataifa ya filamu yanayofahamika kama “Fantasia International film festival” Julai 27, 2019. 

Agosti 21 mwaka huu ikaachiliwa kwa ajili kuonyeshwa katika maeneo mbalimbali duniani kampuni ya kutengeneza filamu ya Walt Disney Motion Pictures ya nchini Marekani. 

Utafanyaje kama wakwe zako wanapoanza kukuwinda kwa silaha badala ya kusherekea harusi yako? Picha|Mtandao.

Filamu hizi tatu ambazo kwa sasa ndiyo zinatikisa soko la filamu zinaoonyeshwa kuanzia leo katika kumbi mbalimbali ukiwemo Century Cinemax ambazo zinapatikana kwenye maduka makubwa “malls” kama Mlimani city, Mkuki House, Aura Mall na Dar Free Market ambazo zipo jijii Dar es Salaam.

Enable Notifications OK No thanks