Filamu hizi zitakusaidia kuondoa msongo wa mawazo
- Filamu hizo ambazo zinaanza kuonyeshwa leo ni “Dora and The Lost City of Gold” pamoja na “Hustlers” yake Jennifer Lopez
- Filamu hizi zote zitaonyeshwa kwa wiki nzima katika kumbi za sinema.
- Unataka kuona visa vya kusisimua vitakavyoamsha hisia zako, usikose filamu hizi.
Dar es Salaam. Filamu ni kati ya burudani ambazo zinaweza kukusaidia kuepukana na msongo wa mawazo na hata kukuburudisha na kukuondolea uchovu.
Kama wewe ni mpenzi wa filamu basi filamu hizi mpya zinazoonyeshwa kwenye kumbi za sinema hapa Jijini Dar es Salaam zikiwemo Mlimani City Mall na Mkuki House Mall zitakufaa.
Dora and The Lost City of Gold
Kwa yeyote anayefuatilia katuni za “Dora the explorer” anafahamu kuwa misitu, wanyama na watu haviwezi kumkwamisha Dora kufikia malengo yake.
Inakuwaje pale Dora anaigizwa na Isabela Moner (“Instant family” na “Transformers”) na sasa, anatakiwa kuwaokoa wazazi wake?.
Je, Michael Peña (Baba Dora) ambaye ni mwigizaji nyota kwenye filamu ya “Ant man” na mama Dora yaani Eva Longoria (Elena) aliyeshiriki filamu zaidi ya 45 zikiwemo “John Wick” (2014) na “Desperate house maids” (2004-2014) wataokolewa kutoka kwenye msitu uliojaa viumbe vya ajabu?
Jibu maswali yako kwa kufuatilia filamu hii uliyogharimu Sh177.5 bilioni chini ya Kiongozi James Bobin ambaye ameongoza filamu kadhaa zikiwemo “Spyz” na “The Muppets”
Zinazohusiana
Waliokua zamani wanenguaji, wanaungana kwa ajili ya kugeuza kibao kwa wateja wao. Pale madili yanapoanza kufanikiwa na wanapoanza kuzishika pesa ambazo hawajawahi kushika, ndipo ubaya unapoinuka.
Filamu hii imesheheni nyota wa muziki kama Jennifer Lopez, Usher, Cardi B na Keke Palmer. Je wasichana hao wataweza kushikilia nafasi ya ubosi kwa muda gani?
Jibu maswali yako kwa kutembelea kumbi za sinema kwa siku saba zijazo kuanzia leo (Septemba 13, 2019).
Pamoa na hayo, kama hujafanikiwa kujua hatma ya “IT”, Angel has Fallen wala “Lion King”? sinema hizo bado zinaonyeshwa kwenye kumbi za Mlimani City, Mkuki House na Dar Free Market.
Latest
