FIFA, WHO waingia ubia kuboresha afya kupitia michezo

October 5, 2019 10:09 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link

Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dk Tedros Adhom Ghebreyesus (kushoto) na Rais wa FIFA, Gianni Infantino wametia saaini mkataba wa ushirikiano kati ya mashirika hayo mawili ili kuhamasisha maisha ya kiafya kupitia mchezo wa mpira wa miguu kimataifa. Picha|WHO.


  • Mashirika yote mawili yameweka ahadi ya miaka minne ya ushirikiano katika kuhamasisha maisha ya kiafya kupitia michezo kimataifa.
  • Wataitumia michezo kusambaza ujumbe wa afya bora kwenda kwa idadi kubwa ya watu.

Shirika la Afya Duniani (WHO) na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) wametangaza ubia katika kukuza uelewa wa faida za kuishi maisha yenye afya kupitia michezo ya kimataifa katika nchi mbalimbali. 

Mashirika yote mawili yameweka ahadi ya miaka minne ya ushirikiano katika kuhamasisha maisha ya kiafya kupitia michezo kimataifa kutokana na uwezo wake wa kusambaza ujumbe kwa kasi na kwa watu wengi zaidi duniani.

Mkataba wa makubaliano ya ubia huo umefanyika jana (Oktoba 4, 2019) makao makuu ya WHO,  Geneva Uswisi. 

Mkurugenzi Mkuu wa WHO, Dk Tedros Adhom Ghebreyesus wakati wa uzinduzi wa ushirikiano huo amesema nusu ya watu wote ulimwenguni walitazama kombe la dunia mwaka 2018, jambo linalotoa fursa ya kutoa elimu ya afya.

“Hii inamaanisha kuwa kuna uwezekano mkubwa kwetu kuungana kuwaafikishia taarifa mabilioni ya watu za kuwasaidia kuishi maisha marefu na yenye afya,” amesema Ghebreyesus.

Juhudi za kuwashawishi mashabiki wa soka kuachana na uvutaji wa sigara itakuwa sehemu ya ushirikiano huo kati ya WHO na FIFA, ambao tayari wana ushirikiano katika kampeni ya kupambana na uvutaji wa sigara ikiwemo katika kombe la dunia la mwaka 2018.


Soma zaidi:  Lucy Protas: Msichana aliyepania kuinua michezo shuleni


WHO itafanya kazi na FIFA kuhakikisha inaweka mazingira ya kutokuwepo kwa sigara katika matukio yatakayoandaliwa na shirikisho hilo la soka, kuhamasisha mashirikisho ya soka ya mataifa kuitekeleza sera ya matukio bila sigara na pia kuwapa FIFA ushauri wa kitaalamu katika usafi na kudhibiti magonjwa.

Kwa kipindi cha miaka miaka minne, programu za pamoja na mipango ya pamoja zinayohusisha vyama vya soka vya mataifa, wachezaji wa mpira, walimu wa soka na wanaojitolea kuhudumu michezoni watasaidia kupata watu kupitia shughuli zinazohusisha mpira wa miguu.

Rais wa FIFA, Gianni Infantino amesema ushirikiano umekuja kwa wakati kwa sababu mpira wa miguu ukitumiwa vizuri unaweza kusaidia kuboresha afya za wananchi wa mataifa mbalimbali.

“Mpira wa miguu ni wa kipekee, ni lugha ya dunia nzima na tunataka kutumia majukwaa yetu na mtandao wetu kuunga mkono mpango wa kiafya na kukuza maisha bora kote ulimwenguni,” amesema Infantino. 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
25 Aug, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
25 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
25 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Elimu ya kodi mwarobaini wa wafanyabiashara kuikwepa TRA, ianzie shuleni

Elimu ya kodi mwarobaini wa wafanyabiashara kuikwepa TRA, ianzie shuleni

Nukta TV

Rais Samia: Serikali chini ya Magufuli haikutaka kuyumbishwa kukamili kwa JNHPP

Rais Samia: Serikali chini ya Magufuli haikutaka kuyumbishwa kukamili kwa JNHPP

Nukta TV

Rais Samia: Umeme wa SGR hautoingiliwa, Dodoma umeme uhakika 24/7

Rais Samia: Umeme wa SGR hautoingiliwa, Dodoma umeme uhakika 24/7

Nukta TV