Fanya haya kuongeza uhai wa betri la ‘laptop’

February 2, 2019 12:26 pm · Zahara
Share
Tweet
Copy Link
  • Mabadiliko ya tabia ikiwemo kupunguza mwanga, kuzima programu zisizotumika yatasaidia betri kudumu kwa muda mrefu.
  • Muhimu ni kufahamu kuwa uwezo wa utendaji wa betri hutofautiana, hata muda kuendelea kufanya kazi utakuwa tofauti.

Dar es Salaam: Matumizi ya vifaa vya kieletroniki yanakuja na gharama zake hasa katika uhifadhi au utunzaji. Hii ni kwasababu visivyotunzwa kuna uwezekano wa kuingia gharama kubwa za matengenezo au kununua kifaa kingine. 

Katika zama hizi za teknolojia, matumizi ya kompyuta mpakato (Laptop) yanashika kasi. Watumiaji wakubwa wamekuwa wafanyakazi maofisini na wanafunzi wa taasisi za elimu, lengo likiwa ni kurahisisha utendaji wa kazi na kuunganishwa na dunia kwa taarifa mbalimbali za maendeleo.

Katika matumizi hayo, wapo ambao wanakumbana na changamoto ya kuharibika haraka kwa betri zinazoipa nguvu kompyuta. Jambo hili limewafanya kutoboa mifuko yao mara kwa mara ili kununua betri mpya.

Lakini umewahi kujiuliza kwanini betri ya kompyuta yako haidumu muda mrefu? Zipo tabia za kibinadamu  zinazosababisha hali hiyo ambazo ukiziacha zinaweza kuliongezea uhai betri ili upate umeme wa kutosha kuendesha kompyuta yako.

Hakikisha kioo cha kompyuta yako kinatumia mwanga wa kawaida ili kupunguza matumizi ya umeme. Kama utatumia mwanga mkubwa (high light) unalifanya betri kutumia nguvu kubwa ili kukidhi mahitaji ya kompyuta. Mwanga mkubwa utumike pale inapohitajika hasa kwenye maeneo yenye giza.

Tumia ‘setting’ za kompyuta yako kupunguza mwanga kulingana na mahitaji yako ili kuhifadhi umeme na kulilinda betri lako lisifanye kazi kupita kawaida. 

Matumizi sahihi ya betri ndiyo siri ya kudumu muda mrefu, jambo linaloweza kukupunguzia gharama za kununua jipya kila mara. Picha| Digital Trends.

Vilevile unashauriwa kuangalia mfumo wa utendaji wa programu za kompyuta yako. Ikiwezekana punguza matumizi ya programu ambazo hazina umuhimu au hazihitajiki kwa kipindi fulani. 

katika ‘settings’ sehemu ya kubadilisha mambo mbalimbali katika kompyuta yako ili uweze kuangalia ni programu gani inatumia zaidi betri la kompyuta ili ujifunze jinsi ya kupunguza matumizi hayo, ili betri lako lidumu kwa muda mrefu.

“Wazime programu ambazo hawazitumii kwenye kompyuta maana zinatabia ya kuendelea kufanya kazi pasipo wewe kujua na kupelekea matumizi ya betri kuwa makubwa,” amesema Khadija Mahanga, Mtaalam wa Programu za kompyuta kutoka kampuni ya Code for Africa (CFA).


Zinazohusiana: Teknolojia 4 zinazoangaziwa zaidi 2019

                           Namna mabadiliko ya teknolojia ‘yalivyozipoteza’ simu za mezani Tanzania


Sambamba na hilo ni kuzima mtandao wa intaneti (Wi-Fi ) hasa pale unapokuwa hauna matumizi nayo, hii ni kwasababu ukiacha wazi ina tabia ya kuendelea kutafuta vitu mtandaoni na wakati huo huo betri lako nalo linatumika kutoa nguvu isiyohitajika kwa wakati huo.   

Pia Wataalamu wanapendekeza kuwa hata wakati ukitumia mtandao usifungue vitu vingi kwa wakati mmoja kwasababu vinaongeza matumizi ya umeme na ni sababu ya kupunguza uhai wa betri la kompyuta. 

“Inabidi watu waache kufungua au kutafuta vitu vingi kwenye mtandao kwa muda mmoja kwasababu sio vyote vinatumika kwa muda mmoja ili kuokoa matumizi ya betri,” amesema George Machibya kutoka kampuni ya teknolojia ya Africa’s Talking.

Muhimu ni kuizima kabisa kompyuta kama huitumii. Wapo watu ambao wanawasha bila sababu yoyote na kuendelea na shughuli zingine siku nzima. Hayo ni matumizi mabaya ambayo yanaathiri uwezo wa betri na utalazimika kununua betri mara kwa mara.

Chaji vizuri betri lako kabla ya kuchomoa waya wa soketi unaingiza umeme kwenye kompyuta ili kulihakikishia nguvu kwa muda mrefu. Picha| Digital Trends.

Betri likijaa yaani likifika asilimia 100, ondoa kwenye soketi ya umeme (charger) ili kuliwezesha kutumia umeme uliohifadhiwa. Hii itakusaidia kupima uwezo wa betri lako katika kuhifadhi umeme. 

Lakini bado unaweza kuamua kuliondoa betri kwenye kompyuta na kutumia umeme moja kwa moja kutoka kwenye soketi ili kuepuka usumbufu wa kulichosha betri. Changamoto yake ni kuwa umeme ukikatika ghafla baadhi ya vitu vinaweza kupotea kwenye kompyuta. 

Mabadiliko ya tabia yanaweza kukusaidia katika kulipa uhai betri lako. Muhimu ni kufahamu kuwa uwezo wa betri hutofautiana kwa maana hiyo hata muda kuishi hutofautiana.

 

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
21 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
21 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
21 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Mwanzo mwisho mapokezi ya Rais wa Namibia Netumbo Nandi Ikulu Dar es Salaam

Nukta TV

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Sikia kisa cha bibi wa Mbagala, chanzo Jaji Mkuu Masaju kupanda cheo

Nukta TV

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

FAHAMU KUHUSU SIKOSELI | Part 1: Ugonjwa wa kurithi, unaotesa maelfu ya watoto Tanzania

Nukta TV