Fahamu: Kujibana pumzi siyo kipimo cha Corona

June 30, 2020 8:17 am · Daniel Samson
Share
Tweet
Copy Link
  • Utathibitishwa hauna Corona ukipata vipimo vya maabara. 
  • Kubana pumzi isitoke kwa sekunde 10 au zaidi bila kukohoa au kujisikia vibaya siyo ishara kuwa uko salama dhidi ya virusi vya Corona.

Dar es Salaam. Iwapo wewe ni miongoni mwa watu wanaoamini habari zinazoeleza kuwa kujibana pumzi isitoke kwa sekunde 10 au zaidi bila kukohoa au kujisikia vibaya ni ishara kuwa uko salama dhidi ya virusi vya Corona, umedanganywa.

Huo ni uzushi wa baadhi ya watu ambao wanatumia mitandao ya kijamii vibaya kupotosha watu kuhusu ugonjwa wa COVID-19. 

​Shirika la Afya Duniani (WHO) linaeleza kuwa dalili kuu za mtu aliyepata COVID-19 ni kikohozi kikavu, uchovu na homa lakini vipimo vya hospitali ndiyo vinathibitisha kama mtu ana ugonjwa huo au la na siyo kujibana pumzi. 

“Njia sahihi ya kuthibitisha kama una virusi vinavyozalisha ugonjwa wa COVID-19 ni kupata kipimo cha maabara,” imeeleza WHO. 


Zinazohusiana


Shirika hilo ambalo linasimamia afya ya dunia limeeleza kuwa huwezi kuthibitisha kama una COVID-19 kwa zoezi la kupumua, jambo ambalo linaweza kukuhatarisha afya yako kuliko kukusaidia. 

Bado unakumbushwa kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa huo kwa kunawa mikono kwa maji tiririka yenye sabuni, kutumia kitakasa mikono na kuvaa barakoa unapoenda kwenye mikusanyiko.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
WORD BANK: Tanzania haina upungufu wa ajira, changamoto tija yake

WORD BANK: Tanzania haina upungufu wa ajira, changamoto tija yake

Nukta TV

CEOs kung'oka baada ya miaka 10, BoT yarudisha mjadala

CEOs kung'oka baada ya miaka 10, BoT yarudisha mjadala

Nukta TV

Onyo la wachumi ikiwa ukomo wa miaka 10 hautoondolewa kwa CEOs wa benki

Onyo la wachumi ikiwa ukomo wa miaka 10 hautoondolewa kwa CEOs wa benki

Nukta TV