Ewura yachangia zaidi ya Sh5 milioni kuboresha huduma za afya Mwanza

February 9, 2023 1:33 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Fedha hizo zitatumika kununua vifaa tiba.
  • Itaongeza ufanisi wa huduma katika hospitali ya Wilaya ya Nyamagana ya Butimba.

Mwanza. Katika kukabiliana na changamoto ya upungufu wa vifaa tiba kwenye hospitali ya Wilaya ya Nyamagana Butimba, Mamlaka ya Uthibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetoa vifaa hivyo vyenye thamani ya Sh5.2 milioni ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wao kwa jamii.

Vifaa vitakavyonunuliwa kwenye hospitali hiyo ni pamoja na mashine sita za kupimia joto, baiskeli za kubebea wagonjwa mbili (Wheel chair), vitanda vya uchunguzi vinne, na vifaa vya kujifungulia akina mama wajawazito (derivery kit) boksi 10 vyote vikiwa na thamani hiyo ya fedha.

Hospital inayoongoza kwa kupokea wagonjwa wengi wanaotoka maeneo mbalimbali wakiongozwa na wanawake wajawazito na wagonjwa wa nje (opd). Ujio wa vifaa hivyo utasaidia kuongeza ufanisi wa matibabu.

Kwa mjibu wa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya jiji la Mwanza, Sebastian Pima amesema takwimu zinaonyesha kuwa kwa wanawake wajawazito kati ya 650 na 750 wanajifungua katika hospitali hiyo, wagonjwa wa nje (Opd) 8,000 hadi 12,000, huku wanawake wajawazito wanaohudhuria kliniki ni 3,500 hadi 5,000.

“Takwimu hizi ni kubwa kwa sababu sera ya afya inataka watoto chini ya miaka mitano na wanawake wajawazito na wanaojifungua watibiwe bure, hivyo msaada huu utaenda kupunguza changamoto iliyokuwepo kwenye hospitali hiyo,” amesema Dk Pima.

Akizungumza kabla ya kukabidhi mfano wa hundi ya Sh5.2 milioni kwa Mganga Mkuu huyo, Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa EWURA, Poline Msuya amesema wameona waunge mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita katika sekta ya afya.

“Imani yetu ni kwamba mchango huo utasaidia kuokoa maisha ya Watanzania na kuboresha huduma ya utoaji afya katika Mkoa wa Mwanza,” amesema Msuya.


Zinazohusiana


Mbali na Msaada huo baraza hilo pia limelenga kujadili mwenendo wa utekelezaji wa huduma za udhibiti wa nishati na maji nchini pamoja na bajeti ya taasisi hiyo katika mwaka wa fedha 2023/24.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Adam Malima, Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi amewataka wafanyakazi hao kutambua wajibu wao na kuzingatia maadili ya utumishi wa umma ili kuleta matokeo chanya ya utendaji wa kazi na wenye tija.

Kuhusu kujadili bajeti ya EWURA, Mkuu huyo wa Wilaya amesema ni ajenda muhimu kwakuwa itatoa mwanga na picha halisi ya utendaji wa Mamlaka kwa mwaka ujao wa fedha.

“Niwaombe mshiriki kikamlifu katika majadiliano hayo na kupitisha bajeti kwa maslahi mapana ya taifa,” amesema Makilagi.

Ametoa amelekezo matatu kwa mamlaka hiyo moja ikiwa ni pamoja na kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi na kasi ya juu kuleta unafuu wa utoaji huduma zenye ubora kwa wananchi katika sekta ya nishati na mafuta.

Amewataka pia kuzingatia uwazi katika upimaji wa utendaji wa wafanyakazi na kuhakikisha utekelezaji wa majukumu unakwenda sambamba  na thamani halisi ya rasilimali zilizopo ili kutokuwepo manung’uniko, ugomvi chuki, husda na majungu mahali pa kazi ambayo yasipodhibitiwa hupelekea utendaji hafifu.

Pia amesisitiza uwajibikaji ipasavyo katika utekelezaji wa majukumu yao sanjari na kufuata maadili ya utumishi wa umma kuwa na nidhamu, utii na heshima wakati wote wa utendaji wao.

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: LIVE:WABUNGE WAKIWACHAPA MASWALI MAWAZIRI | Bunge la 13 | Kikao cha 28

🔴LIVE: LIVE:WABUNGE WAKIWACHAPA MASWALI MAWAZIRI | Bunge la 13 | Kikao cha 28

Nukta TV

Top 10 ya magari yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta

Top 10 ya magari yanayotumia kiwango kidogo cha mafuta

Nukta TV

SGR yaingizia Serikali Sh169.37 bilioni tangu kuanza kwa safari Juni 2024

SGR yaingizia Serikali Sh169.37 bilioni tangu kuanza kwa safari Juni 2024

Nukta TV