Dola ya Marekani tulivu dhidi ya Shilingi ya Tanzania
Dar es Salaam. Dola ya Marekani imeendelea kuonesha utulivu dhidi ya Shilingi ya Tanzania, kwa mujibu wa viwango vya kubadilisha fedha vilivyotolewa na Benki ya CRDB na NMB leo Novemba 4, 2026.
Leo benki ya CRDB, dola moja inanunuliwa kwa Sh2,600 na kuuzwa kwa Sh2,680 ikiwa ni sawa na nviwango vilivyotumika Septemba 15, 2026.
Kwa upande wa NMB, dola moja inanunuliwa kwa Sh2,590, kutoka Sh2,595 mwezi Septemba, huku ikiuzwa kwa Sh2,670, kutoka Sh2,675.
Mabadiliko hayo madogo yanaashiria kuendelea kwa utulivu wa Dola ya Marekani dhidi ya Shilingi ya Tanzania, bila kuwepo kwa mabadiliko makubwa katika kipindi hicho.
