Brela yaongeza siku 90 usajili kampuni, majina ya biashara kielektroniki

January 2, 2020 9:59 am · TULINAGWE ALSON
Share
Tweet
Copy Link
  • Kuongezwa kwa muda huo kunakuja baada ya ule wa awali uliowekwa kumalizika.
  • Sasa wanaofanya usajili wanatakiwa kukamilisha zoezi hilo kabla ya Machi 31, 2020. 
  • Unahusu makampuni na majina ya biashara zilizosajiliwa nje ya mfumo wa kielektroniki unaotumika sasa.

Dar es Salaam. Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) umeongeza siku 90 kwa makampuni na majina biashara zilizosajiliwa nje ya mfumo wa kielektroniki unaotumika sasa kuuhuisha taarifa zao kabla ya muda huo kumalizika ili kuhakikisha taarifa hizo zinakuwepo katika mfumo wa pamoja. 

Hatua hiyo inakuja baada ya muda uliowekwa awali wa miezi mitatu ambao umemalizika mwishoni mwa mwaka 2019 kupita ili kutoa fursa kwa wale ambao hawakukamilisha zoezi hilo kwa wakati kutokana na sababu mbalimbali. 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Brela jana (Januari 1, 2020) katika ukurasa wake wa Twitter inaeleza kuwa makampuni na majina ya biashara yaliyosajiliwa nje ya mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao (Online Registration System – ORS) ambayo bado hayafanya hivyo, yanatakiwa kukamilisha usajili kabla ya Machi 31, 2020.

“Brela inawataka wadau wote waliosajili makampuni na majina ya biashara nje ya mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao (ORS) kukamilisha zoezi hilo ndani ya muda ulioanishwa,” inaeleza sehemu ya taarifa iliyotolewa na Afisa Habari na Mawasiliano wa Brela, Robertha Makinda. 

​Katika uhuishaji huo, yapo mambo ya muhimu ya kuzingatia ikiwemo kuwa na namba ya kitambulisho cha utaifa (NIDA) na namba ya utambulisho wa mlipa kodi (TIN)

Pamoja na hayo, muombaji anatakiwa kupitia taarifa za kampuni na kuhakikisha zipo sahihi kisheria na kikanuni  pamoja na kujaza fomu katika mfumo wa kielektroniki wa ORS (Online Registration System) na kupakia taarifa zote zinazohitajika zikiwemo taarifa ya mwaka (Annual Returns), mabadiliko yaliyotokea katika kampuni ambayo hayakuwasilishwa awali.

Muombaji pia anatakiwa kuhakikisha kuweka saini kwenye fomu zote ikiwemo na kisha kuzipakia kwenye akaunti na kuzitazama Brela kwa njia ya mtandao.


Zinazohusiana:


Msisitizo uliotolewa na Brela ni pamoja na kuwasilisha taarifa sahihi zinazoendana na taarifa zilizopo masijala ya usajili, kufanya zoezi kwa ueledi na ikibidi kuhusisha watu wenye uelewa wa sheria za usajili, kuwasilisha taarifa kamili na kuzingatia maelekezo ya marekebisho kwenye maombi yanayorudishwa.

Samabamba na hilo, atakayefungua akaunti kwenye mfumo wa usajili kwa njia ya mtandao atakuwa yule mwenye hisa kwenye kampuni au mmiliki wa jina la biashara husika.

May 10, 2018, wakala huo ulizindua mfumo wa kielektroniki wa usajili wa kampuni na biashara na huduma nyingine ikiwemo nembo ya biashara, bidhaa au huduma pamoja na utoaji wa leseni mbalimbali. 

Huo ni muendelezo wa uhuishwaji wa taarifa za makampuni na majina ya biashara ili kuhakikisha taarifa hizo zinakuwepo katika mfumo wa kielektroniki ambao ni rahisi na uhakika katika kutunza kumbukumbu.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
13 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
13 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
13 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

🔴LIVE: HII HAPA BAJETI KUU YA SERIKALI 2026/2027

Nukta TV

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Mashine za kukaushia rangi za kucha kutozwa ushuru kwa asilimia 10

Nukta TV

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Wazee wa 'kubet' hii inawahusu, 5% kutozwa kwenye dau la kamari

Nukta TV