Bodaboda, bajaji kushushiwa adhabu za barabarani Tanzania

June 10, 2021 2:27 pm · Mariam John
Share
Tweet
Copy Link
  • Adhabu hizo zinapendekezwa kushushwa mara tatu kutoka Sh30,000 kwa kosa moja hadi Sh10,000.

Mwanza. Serikali ya Tanzania inapendekeza kupunguza adhabu za usalama wa barabarani kwa makosa ya pikipiki na bajaji mara tatu kutoka Sh30,000 hadi Sh10,000.

Iwapo pendekezo hilo litapitishwa na bunge, litatoa ahueni kwa wamiliki wa vifaa hivyo moto vinavyotumiwa zaidi vijana kama sehemu ya ajira.

Waziri wa Fedha na Mipango Dk Mwigulu Nchemba amesema leo bungeni wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Serikali mwaka 2021/22 kuwa vijana wengi wamejiajiri kwenye sekta ndogo ya kuendesha bajaji na pikipiki zikijulikana kama bodaboda.

Dk Nchemba amesema pamoja na kujishughulisha na kazi hizo, vijana hao hupata usumbufu mkubwa wa kulipa faini kutoka kwenye vipato vyao pale panapotokea uvunjaji wa Sheria ya Usalama Barabarani umefanywa na abiria wao.

Ukosefu wa fedha za kulipa adhabu hizo, umesababisha baadhi yao kushindwa kulipa faini na hivyo kuzitelekeza pikipiki zao kwenye vituo vya polisi.

“Mheshimiwa Rais alielekeza jeshi la Polisi kujikita kwenye kutoa elimu kuhusu usalama barabarani badala ya kuwekeza kwenye makosa na kugeuza faini kuwa chanzo cha mapato,” amesema Dk Nchemba na kuongeza;

“Hivyo basi, napendekeza kupunguza adhabu zinazotolewa chini ya Sheria ya Usalama Barabarani SURA 168 kwa makosa ya Pikipiki na Bajaji kutoka Sh30,000 za sasa hadi Sh10,000 kwa kosa moja.”

Lengo la hatua hiyo, amesema, ni kuweka adhabu kwa kuzingatia uwezo wa kulipa.

Hata wakati Serikali ikipendekeza nafuu hiyo ya adhabu, Dk Nchemba ameeleza kuwa adhabu za makosa mengine ya vyombo vya moto zinazotolewa kwa mujibu wa Sheria zinaendelea kubaki kama ilivyo sasa.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
14 Jun, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
15 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
15 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Mwenendo wa deni la serikali

Mwenendo wa deni la serikali

Nukta TV

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Rais Samia: Uchumi wa nchi unapanda , lakini ukifika kwa watu hali si nzuri

Nukta TV

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Gavana Tutuba afichua kiasi cha dhahabu kilichopo BoT thamani yake

Nukta TV