Bidhaa za bia, juisi za unga kutozwa ushuru 2020-21

June 11, 2020 2:13 pm · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Bidhaa hizo ni juisi na bia za unga zinazoingizwa kutoka nje ya nchi
  • Bidhaa ya juisi zinapendekezwa kutozwa zaidi ya Sh 232 huku bia za unga zikipendekezwa kutozwa zaidi ya Sh800.

Dar es Salaam. Waziri wa Fedha na Mipango Dk Philip Mpango amependekeza kufanya marekebisho ya kutoza ushuru wa bidhaa za  bia na juisi za unga ambazo zinaingizwa kutoka nchi za nje.

Amesema lengo la mabadiliko hayo ni kupanua wigo wa kodi kwa kuwa bidhaa hizo zinaagizwa kwa wingi kutoka nje ya nchi.


Zinazohusiana


Kwa upande wa bia za unga, waziri huyo amependekeza bidhaa hiyo itozwe ushuru kwa kiwango cha Sh844 kwa kilo na juisi ya unga (Sh232)

“Hatua za kutoza ushuru wa bidhaa kwenye bidhaa zisizo za petroli kwa ujumla wake zinatarajiwa kuongeza mapato ya Serikali kwa kiasi cha shilingi bilioni 45.8,” amesema Dk Mpango leo wakati akiwasilisha bajeti kuu ya Serikali ya mwaka 2020/21. 

Enable Notifications OK No thanks