Benki, hoteli za kitalii kutumika kubadilishia fedha Jijini Arusha-BoT

November 25, 2018 1:01 am · Rodgers Raphael
Share
Tweet
Copy Link
  • Uamuzi huo unakuja  baada ya wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara ya kubadilisha fedha za kigeni kutakiwa kurudisha leseni kwa kile kinachodaiwa baadhi yao wameshindwa kukidhi vigezo vya kuendesha biashara hiyo.
  • Sambamba na hilo BoT imesitisha utoaji wa leseni za biashara ya ubadilishaji fedha kwa takribani miezi mitatu sasa na kusimamisha upokeaji wa maombi mapya mpaka taratibu mpya zitakapokamilika.

Dar es Salaam. Benki kuu ya Tanzania (BoT) imetaja sehemu rasmi za kubadilishia fedha za kigeni jijini Arusha kuwa ni hoteli za kitalii pamoja na benki za biashara.

Uamuzi huo unakuja baada ya wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara ya kubadilisha fedha kutakiwa kurudisha leseni kwa kile kinachodaiwa baadhi yao kushindwa kukidhi vigezo vya kuendesha biashara hiyo.

Pia BoT ililazimika kutumia askari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) katika oparesheni ya kukagua maduka ya ubadilishaji fedha jijini humo Novemba 19, 2018 jambo lililoibua mjadala na sintofahamu ya jeshi hilo kuhusika katika shughuli ambazo zilipaswa kufanywa na taasisi husika

Sambamba na hilo BoT imesitisha utoaji wa leseni za biashara ya ubadilishaji fedha kwa takribani miezi mitatu sasa na kusimamisha upokeaji wa maombi mapya mpaka taratibu mpya za uendeshaji wa biashara hiyo zitakapokuwa tayari.


Zinazohusiana:


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Dk Bernard Kibesse, hatua hiyo imefikiwa baada ya kufanyika ukaguzi wa kushitukiza jijini Arusha ulio baini uwepo wa maduka ya kubadilishia fedha yanayokiuka taratibu na sheria za biashara ya kubadilisha fedha.

“Benki Kuu ya Tanzania ilifanya ukaguzi wa ghafla katika maduka ya kubadilishia fedha jijini Arusha tarehe 19 Novemba 2018 na kuamua kuyafunga maduka yasiyozingatia taratibu na sheria,” amesema Dkt Kibesse.

Aidha, huduma ya kubadilisha fedha imebaki ikipatikana kwenye maduka ya kubadilishia fedha za kigeni, hoteli za kitalii pamoja na benki za biashara kote nchini.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
26 Jul, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
26 Jul, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
26 Jul, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Hizi ndio passport 5 zenye nguvu zaidi duniani

Nukta TV

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Hii ndio spirulina: Hazina ya maji inayoboresha afya za Watanzania

Nukta TV

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Mradi wa Sh4.6 bilioni kutoa ahueni ya umeme Lindi, Mtwara

Nukta TV