Bei ya maharage yang’ang’ania kiwango cha Jumatano
- Bei ya juu ya gunia la kilo 100 la maharage inauzwa kwa Sh270,000 katika masoko ya Tandika na Kinondoni jijini Dar es Salaam.
- Bei ya chini ya zao hilo imerekodiwa katika mikoa ya Rukwa, Kagera na Manyara ambako gunia la kilo 100 kwa Sh120,000.
- Bei hizo hazijabadilika tangu Jumatano Machi 25, 2020.
Dar es Salaam. Bei ya juu na chini ya maharage inayotumika leo katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania imeendelea kubaki katika kiwango kile kile kilichorekodiwa jumatano Machi 25, 2020.
Kwa mujibu wa takwimu za mazao makuu ya biashara zilizotolewa leo (Machi 27, 2020) na Wizara ya Viwanda na Biashara zinaeleza kuwa bei ya juu ya gunia la kilo 100 la maharage inauzwa kwa Sh270,000 katika masoko ya Tandika na Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Bei hiyo inayotumika leo ilitumika pia Jumatano Machi 25, 2020 katika soko la Tandika jijini Dar es Salaam.
Wakati bei ya juu ya maharage ikirekodiwa Dar es Salaam, bei ya chini ya zao hilo imerekodiwa katika mikoa ya Rukwa, Kagera na Manyara ambako gunia la kilo 100 inauzwa kwa Sh120,000.
Bei hiyo haijabadilika inaendelea kutumika kama ilivyokuwa Jumatano katika mikoa ya Manyara na Kagera.
Ifahamike kuwa utaratibu wa kutoa bei za jumla za mazao makuu ya chakula hufanyika mara tatu kwa wiki yaani Jumatatu, Jumatano na Ijumaa.