Bajeti Wizara ya Katiba na Sheria yapaa kwa asilimia 40.6

April 25, 2023 11:51 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Imeongezeka kutoka Sh272.7 bilioni ya mwaka 2022/23 hadi Sh383,6 bilioni kwa mwaka 2023/24.
  • Bajeti hiyo ina vipaumbele 19 ikiwemo mchakato wa Katiba Mpya. 
  • Mabadiliko ya Sheria za Uchaguzi na Demokrasia pia yamo. 

Dar es Salaam. Wizara ya Katiba na Sheria imeliomba Bunge kuidhinisha bajeti ya Sh383,6 bilioni kwa mwaka 2023/24 huku ikiainisha vipaumbele 19 ikiwemo kuratibu na kutoa elimu ya mchakato wa Katiba Mpya. 

Ikiwa bajeti hiyo itapitishwa na Wabunge leo Aprili 25, 2023 itakuwa imeongezeka kwa asilimia 40.6 kutoka Sh272.7 bilioni ya mwaka 2022/23.

Kwa mujibu wa Waziri wa wizara hiyo, Dk Damas Ndumbaro, katika kipindi cha Julai, 2022 hadi Machi, 2023, wizara imepokea Sh187.4 bilioni sawa na asilimia 68.7 ya fedha zote zilizoidhinishwa katika mwaka wa fedha 2022/23. 

Kati ya hizo, Sh62.7 bilioni ni mishahara sawa na asilimia 66 ya bajeti yote na Sh83.1 bilioni ni matumizi mengineyo. 

Fedha za maendeleo zilizopokelewa ni Sh41.6 bilioni sawa na asilimia 64 ya fedha zilizoidhinishwa ambazo zinajumuisha Sh35.4 bilioni fedha za ndani. 

Waziri Ndumbaro amesema kati ya Sh383,6 bilioni zinazoombwa, Sh109.6 bilioni ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo huku kiasi kilichobaki kitaelekezwa katika kulipa mishahara ya watumishi na matumizi mengineyo ya wizara hiyo. 

Waziri wa Katiba na Sheria Dk Damas Ndumbaro akihutubia akiwajibu maswali ya Wabunge katika moja ya vikao vya Bunge. Picha | UDSM.

Vipaumbele 19 vya wizara

Katika mwaka wa fedha 2023/24, Dk Ndumaro amesema wizara na taasisi zake zitaendelea kuboresha utoaji wa huduma za sheria na utoaji haki kwa umma ili kuendana na mipango yake na hivyo kufikia malengo yaliyopangwa kwa kipindi husika. 

Kazi kubwa itakuwa ni kuratibu mchakato wa Katiba Mpya, kutekeleza mkakati wa kutoa elimu ya Katiba kwa umma na kutekeleza kampeni ya ‘Mama Samia Legal Aid Campaign’ kwa wananchi kote nchini.

“Tutafanya marekebisho ya Sheria za Uchaguzi na Demokrasia, tuwasilisha taarifa kwenye vikao 16 na majukwaa ya haki za binadamu na watu katika ngazi ya kikanda na kimataifa,” amesema Waziri Ndumbaro. 

Itakumbukwa Oktoba 21, 2022 Rais Samia akipokea ripoti ya kikosi kazi alichokiunda kwa ajili ya Kuratibu Maoni ya Wadau wa Demokrasia ya Vyama Vingi vya Siasa nchini Tanzania alisema mchakato wa mabadiliko ya Katiba uendelee hatua kwa hatua licha ya kuwa suala lake linahitaji muda.

Pia alisema mabadiliko ya sheria zinazohusu uchaguzi yanaweza kufanyika kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2025. 

Vipaumbele vingine ni kutekeleza programu ya kutumia lugha ya Kiswahili katika utoaji haki nchini, kuwasilisha taarifa tatu za nchi kuhusu utekelezaji wa mikataba mitatu ya haki za binadamu ambayo Serikali imeridhia.

Kuendelea kutafsiri sheria za nchi kutoka lugha ya Kingereza kuwa katika lugha ya Kiswahili na kuimarisha mifumo ya utoaji haki ili haki ipatikane kwa wote na kwa wakati. 


Soma zaidi:


Wizara itaimarisha mifumo ya utatuzi wa migogoro kwa njia mbadala kwa kuanzisha na kuendesha Kituo cha Kimataifa cha Utatuzi wa Migogoro na  mfumo wa elimu ya sheria.

“Tutaratibu mapitio na marekebisho ya sheria za sekta ya sheria, tutandaa sera mahsusi zinazosimamia mifumo ya utoaji haki na kuendelea kuimarisha mfumo wa uangalizi wa utajiriasili na maliasilia za nchi,” amesema waziri huyo.

Pia katika kipindi hicho, wizara itaimarisha matumizi ya Tehama katika utoaji wa huduma za sheria nchini, kuendelea na ujenzi wa vituo jumuishi vya taasisi za sheria, kutoa elimu kwa wananchi kuhusu masuala ya kikatiba na utawala wa sheria.

Kuendelea kuhamasisha matumizi ya njia mbadala za utatuzi wa migogoro ambazo ni usuluhishi, upatanishi, maridhiano na majadiliano ili kurahisisha na kuharakisha upatikanaji wa haki nchini na kuimarisha mifumo ya kuhamasisha, kuzingatia na kulinda haki za binadamu na watu.

Mesema pia watatekeleza Mkakati wa Pili wa Taifa wa Haki Mtoto 2020/21-2024/25 na kuendelea kuimarisha usajili wa matukio muhimu ya binadamu na takwimu pamoja na shughuli za ufilisi na udhamini. 

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria, Abdullah Mwinyi ameishauri Serikali kutoa fedha kwa wakati ili kuiwezesha wizara hiyo kutekelezwa kwa wakati majukumu yake.

Mwinyi amesema iendelee kuimarisha mfumo wa utoaji haki nchini ikiwemo kujenga na kuboresha miundombinu ya mahakama katika maeneo mbalimbali nchini. 

/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Jun, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Jun, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Wabunge waliokwenda Morocco bila kibali kikaangoni , utoro ukiibuliwa bungeni

Nukta TV

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Mfahamu Leonard Mususa Alama ya Ungozi iliyoacha majonzi kwa 'MACEOs' Tanzania

Nukta TV

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Bei za mafuta mwezi Juni hizi hapa, dizeli ikipaa kwa Sh85

Nukta TV