Athari za hewa chafu: Takriban watu milioni 6.5 wafariki dunia

September 8, 2022 4:22 am · Davis Matambo
Share
Tweet
Copy Link
  • Vifo hivyo vya mapema vinakadiriwa kutokea mwaka 2016.
  • UN yataka hatua za haraka kudhibiti uchafuzi wa hewa.

Dar es Salaam. Kwa mara ya tatu siku ya Kimataifa ya Hewa Safi kwa Anga ya Bluu inafanyika Septemba 7, huku wadau wakishauri hatua zaidi zichukuliwe ili kupunguza vifo vinavyotokana na uchafuzi wa hewa.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa (UN) takriban vifo milioni 6.5 vya mapema  vya watu vilitokea mwaka 2016 ulimwenguni kote kutokana na uchafuzi wa hewa wa ndani ya nyumba na nje.

Vifo hivyo vinaweza kuongezeka kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2050 endapo hatua za kudhibiti uchafuzi wa hewa hazitachukuliwa. 

Uchafuzi wa hewa huathiri vibaya wanawake, watoto na wazee, hasa katika nchi zinazoendelea kutokana na nishati ya kuni, mkaa na mafuta ya taa.

Hewa chafu hupenya ndani ya mapafu na mkondo wa damu na hivyo kuathiri utendaji wa mwili. Athari anazoweza kupata mtu ni pamoja na kiharusi, magonjwa sugu ya kupumua, na saratani ya mapafu na mshtuko wa moyo.

Kutokana na athari hizo, UN imesisitiza uwajibikaji na hitali la hatua za pamoja kukabiliana na uchafuzi wa hewa duniani kwa kudhibiti shughuli za viwanda na ukataji miti hovyo. 

Pia inaangazia haja ya ushirikiano wa haraka na wa kimkakati wa kimataifa na kikanda kwa ajili ya utekelezaji bora zaidi wa sera na hatua za kukabiliana na uchafuzi wa hewa.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Aug, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Aug, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
NISHATI

NISHATI

Nukta TV

Utani wa Rais Samia kwa wachimba madini wa Katoro

Utani wa Rais Samia kwa wachimba madini wa Katoro

Nukta TV

Rais Samia: Misaada imepungua, tukaze buti

Rais Samia: Misaada imepungua, tukaze buti

Nukta TV