ATCL kuanza safari za kwenda Mumbai, India leo

July 17, 2019 5:02 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Kwa mujibu wa shirika hilo, safari kwanza itakuwa leo (Julai 17, 2019) na ya pili itakua Juali 19 kwenda moja kwa moja Mumbai.

Dar es Salaam. Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) leo linaanza safari ya kwenda katika jiji la Mumbai nchini India ikiwa ni hatua muhimu ya shirika hilo la umma kujitanua katika utoaji wa huduma za usafiri wa anga kimataifa. 

Safari hiyo mpya inakuja ikiwa zimepita zaidi ya wiki mbili tangu ATCL ilipozindua safari zake kutoka Tanzania hadi katika jiji la Johannesburg nchini Afrika Kusini

Kwa mujibu wa shirika hilo, safari kwanza itakuwa leo (Julai 17, 2019) na ya pili itakua Juali 19 kwenda moja kwa moja Mumbai. 

“Tunafurahi kutangaza kwamba safari yetu ya kwanza tarehe 17 kwenda Mumbai na ya Pili tarehe 19 Julai 2019 tutatumia uwanja mpya wa Julius Nyerere wa safari za kimataifa Terminal 3,” unasomeka ujumbe uliowekwa katika ukurasa wa Twitter wa ATCL.

Kwa anayetaka kusafiri hadi Mumbai, sasa atalipa dola za Marekani 378 sawa na takriban Sh869,232.

Hata hivyo, ATCL itakuwa na kibarua kigumu cha kuboresha huduma zake na kujiimarisha ili kuhimili ushindani wa mashirika makubwa ya Kenya Airways na Ethiopia Airlines ambayo yametawala soko la usafiri wa anga Afrika.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
24 Sep, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
24 Sep, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
24 Sep, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
Ukweli kuhusu Mama Fatma Karume, mwanamke aliyeshika kiganja cha historia ya Zanzibar

Ukweli kuhusu Mama Fatma Karume, mwanamke aliyeshika kiganja cha historia ya Zanzibar

Nukta TV

Tanzania yasisitiza amani na suluhu Mashariki ya Kati, kikao cha 81 cha UN

Tanzania yasisitiza amani na suluhu Mashariki ya Kati, kikao cha 81 cha UN

Nukta TV

Rais Mwinyi: Wananchi wanataka viongozi walete maendeleo, si malumbano ya kisiasa

Rais Mwinyi: Wananchi wanataka viongozi walete maendeleo, si malumbano ya kisiasa

Nukta TV