Apps zinazoweza kukusaidia unapokuwa safarini
- Apps hizo ni pamoja na DUFL ambayo inatoa huduma ya kukupangia na kukubea mizigo mpaka eneo utakalofikia.
- Apps hizo zinawarahisishia wasafiri na kuwafanya wajisikie vizuri wawapo safarini.
Huenda wewe ni mmoja ya watu wanaopendelea kusafiri katika maeneo mbalimbali ili kujionea fahari ya dunia lakini kufanikisha shughuli zako za kikazi na biashara.
Lakini unachofikiria kufanya ukiwa safarini, teknolojia inakupa suluhisho na kukurahisishia zaidi maisha ili kusudi la safari yako litimie kama ulivyopanga.
Kutana na programu tumishi za simu (Apps) zitakazokusaidia kufanikisha mambo mbalimbali ukiwa safarini ikiwemo kukumbusha vitu muhimu unavyopaswa kubeba kwa kila safari unayoiendea:
Ni moja ya programu inayomuondolea usumbufu wa mtu kufikiria ni nini anatakiwa kuwa nacho au kubeba pindi anapokua safarini.
Programu hii inafanya kazi kwa kumwezesha mtu kufanya maamuzi kulingana na mahali atakapokwenda, shughuli atakayokua akifanya na muda atakaotumia safarini.
Inapatikana katika mfumo wa ‘Android pamoja na iOS ambapo inamsaidia mtu kufahamu vitu muhimu vya kubeba. Mfano mtu anaenda kutalii katika mbuga za wanyama, itamkumbusha kubeba kofia, nguo nyepesi na hata dawa za kujikinga na wadudu anapokua mbugani.
Teknolojia inakupa suluhisho na kukurahisishia zaidi maisha unapokua safarini. Picha| Mtandao.
Hii ni programu nyingine ambayo inaweza kutumiwa na simu zenye mfumo wa ‘Android’ na iOS.
Inampa mtu uwezo wa kuwa na msaidizi binafsi (Personal assistant) kwa maana nyingine inatoa huduma ambazo anapaswa kutoa msaidizi wako unapokuwa safarini.
Programu hiyo inayotumika zaidi Uingereza inatoa huduma za kumtafutia mtu usafiri wa ndege na kumfanyia “booking” mpaka mahali anapokwenda lakini vile vile kumtafutia sehemu ya malazi anapoweza kwenda kufikia pindi atakapokua safarini.
Pindi mtu anapochagua usafiri wa kutumia katika kufika mahali anapokwenda kigezo cha nauli atakayotumia ni miongoni mwa mambo muhimu anayozingatia wakati akipanga bajeti yake.
Programu hii ni mahususi kwa watu wanaotumia usafiri wa ndege. Inamsaidia mtu kufahamu bei za ndege mbalimbali, jambo linalomuwezesha kulinganisha na kuchagua bei inayolingana na mfuko wake.
Zinazohusiana
- Apps 10 za kilimo zinazoweza kuwanufaisha wakulima Tanzania
- Apps za elimu zitakazowasaidia wanafunzi 2019
Grab
Inafanya kazi kama Uber na Bolt zinazotoa huduma ya taxi mtandaoni. Inatumika zaidi nchini Singapore, kama una mpango wa kutembelea nchi hiyo ni vema kuipakua kwenye simu yako ili ukifika usipate usumbufu wa kutafuta usafiri wa binafsi na taxi kukupelekea katika hoteli utakayofikia.
Licha ya kutoa huduma za usafiri mtandaoni, pia inasadia kukufikishia chakula ukipendacho popote ulipo kwa miji ya nchi hiyo huku ukifanya malipo kwa njia ya kadi na hata simu.
Wakati mwingine unaweza kukosa muda wa kuandaa vitu vyako au mahitaji utakayotumia safarini.
Basi DUFL wanakurahisishia kwa kupatia sanduku unaloweza kuweka vitu vyako vyote na kukufikishia kule unakokwenda bila usumbufu wowote. Programu hii inawafaa zaidi watu wasiopenda kubeba mizigo mingi.
Licha ya kukufikishia mzigo wako unakataka ufike, wanakupangia vizuri na kama ni nguo basi wanafua na kuzinyoosha vizuri.
Hizo ni baadhi ya programu zinazoweza kumsaidia msafiri pindi anapotaka kusafiri au pale anapojiandaa kwa ajili ya kusafiri zake za masafa marefu au mafupi.