Ahueni kwa wananchi, bei ya maharage ikishuka

April 6, 2020 11:23 am · Mwandishi
Share
Tweet
Copy Link
  • Ni bei ya juu na ya chini ya gunia la kilo 100 inayotumika katika meneo mbalimbali nchini. 
  • Bei ya juu imeshuka kutoka Sh300,000 wiki iliyopita hadi Sh280,000 inayotumika leo jijiji Dar es Salaam.
  • Bei ya chini nayo imeshuka hadi Sh75,000 katika Mkoa wa Rukwa kutoka Sh120,000 iliyorekodiwa wiki iliyopita. 

Dar es Salaam. Bei ya jumla ya maharage imeshuka kwa viwango tofauti ndani ya wiki moja katika mikoa miwili ya Dar es Salaam na Rukwa, jambo linalowapa ahueni wanunuzi wa zao hilo la chakula. 

Maharage ni miongoni mwa mazao makuu ya chakula ambayo hujumuisha mchele, viazi mviringo, mahindi, mtama, uwele, ulezi na ngano.

Takwimu za Wizara ya Viwanda na Biashara zilizotolewa leo (Aprili 6, 2020) zinaeleza kuwa bei ya juu ya gunia la kilo 100 la zao hilo inayotumika leo Dar es Salaam ni Sh280,00 katika soko la Tandika wilayani Temeke. 

Bei hiyo imeshuka kutoka Sh300,000 iliyorekodiwa Jumatatu Machi 30, 2020 jijini humo na hivyo kuwafanya wafanyabiashara wapoteze Sh20,000 kwa kila gunia moja na kuwafaidisha zaidi wanunuzi.

Pia bei ya chini ya zao hilo nayo imeshuka kutoka Sh120,000 iliyorekodiwa wiki iliyopita hadi Sh75,000 inayotumika leo katika Mkoa wa Rukwa. 

Bei za maharage nchini zimekuwa za kupanda na kushuka kulingana na upatikanaji wa zao hilo katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
5 Oct, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
5 Oct, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
WORD BANK: Tanzania haina upungufu wa ajira, changamoto tija yake

WORD BANK: Tanzania haina upungufu wa ajira, changamoto tija yake

Nukta TV

CEOs kung'oka baada ya miaka 10, BoT yarudisha mjadala

CEOs kung'oka baada ya miaka 10, BoT yarudisha mjadala

Nukta TV

Onyo la wachumi ikiwa ukomo wa miaka 10 hautoondolewa kwa CEOs wa benki

Onyo la wachumi ikiwa ukomo wa miaka 10 hautoondolewa kwa CEOs wa benki

Nukta TV