Waandishi wawili wa Nukta Africa wafuzu kuwania Tuzo za Samia Kalamu 2026

November 17, 2026 5:08 pm · Fatuma Hussein
Share
Tweet
Copy Link
  • Daniel Samson na Esau Ng’umbi ni miongoni mwa wanahabari 64 waliofuzu.
  • Washindi watatangazwa Desemba 5, 2026, katika hafla itakayohudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Dar es Salaam. Waandishi wawili wa kampuni ya habari na teknolojia ya Nukta Africa wamefuzu kuwania Tuzo za Samia Kalamu 2026, zinazolenga kutambua ubora na mchango wa wanahabari katika kuandika habari na makala za maendeleo nchini.

Waandishi hao ni Daniel Samson, Mkuu wa Mafunzo wa Nukta Africa, na Esau Ng’umbi, aliyewahi kuwa Mratibu wa Dawati la Habari katika kampuni hiyo ambao wameingia katika orodha ya wanahabari 64 na vyombo vya habari 11 vilivyofuzu kuwania tuzo hizo.

Peter Mwasalyanda, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA), na Mwenyekiti wa Tuzo hizo, aliyekuwa akizungumza na wanahabari leo Novemba 17, 2026 jijini Dar es Salaam amesema washindani waliofuzu walipatikana kupitia mchakato uliohusisha kura za umma na tathmini ya majaji.

“Washindani waliofuzu wamepatikana kupitia mchakato wa upigaji kura wa umma na tathmini ya majaji 19 waliobobea katika taaluma za uandishi wa habari, mawasiliano kwa umma na uhusiano wa umma,” amesema Mwasalyanda.

Tuzo hizo zimegawanywa katika makundi matatu ambayo ni Tuzo za Kisekta, Tuzo kwa Vyombo vya Habari na Tuzo Maalumu za Kitaifa.

Kwa Nukta Africa, huu ni mwaka wa pili kushiriki katika tuzo hizo. Katika msimu wa kwanza uliofanyika mwaka 2025, kampuni hiyo iliwakilishwa na Esau Ng’umbi, ambaye pia amefanikiwa kufuzu kuwania tuzo katika msimu huu. 

Kwenye picha ya pamoja Mkurugenzi Mtendaji wa Nukta Africa, Nuzulack Dausen akiwa na washindi wa tuzo kutoka Nukta Africa. Picha|Nukta Africa.

Rais Samia kuhudhuria hafla ya utoaji tuzo

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya kutangaza na kuwatunuku washindi itakayofanyika Desemba 5, 2026, katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.

Kulingana na Mwasalyanda, jumla ya kazi 3,003 ziliwasilishwa kuwania tuzo hizo. Kati ya hizo, kazi 882 zilifaulu tathmini ya awali na kuingia katika hatua ya upigaji kura wa umma, ambapo kura 317,399 zilipigwa.

Mwasalyanda amesema tuzo hizo zimeanzishwa kutoa nafasi kwa waandishi wa habari, maafisa habari na vyombo vya habari kuonesha ubora wa kazi zao zilizochapishwa au kurushwa hewani ndani ya kipindi kilichobainishwa kwenye mwongozo wa tuzo.

Samia Kalamu Awards (SKA) ni jukwaa la kitaifa lililoanzishwa mwaka 2024 kwa lengo la kutambua na kuhamasisha weledi, ubunifu na ubora katika uandishi wa habari na utayarishaji wa makala za maendeleo nchini.

Daniel Samson, Mkuu wa Mafunzo wa Nukta Africa akipokea tuzo. Picha|Daniel Samson

Toleo la kwanza la tuzo hizo lilifanyika mwaka 2025, huku mwaka huu ukiwa ni msimu wa pili. 

Tuzo hizo zinaandaliwa na TCRA kwa kushirikiana na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) na Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB).

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
17 Nov, 2026 · TZS
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
17 Nov, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
17 Nov, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
JKT: Nafasi haziuzwi, hakuna upendeleo wala kurudia mafunzo

JKT: Nafasi haziuzwi, hakuna upendeleo wala kurudia mafunzo

Nukta TV

Noti za Sh1,000 na Sh2,000 kuchakaa haraka, nini kifanyike? wananchi wafunguka

Noti za Sh1,000 na Sh2,000 kuchakaa haraka, nini kifanyike? wananchi wafunguka

Nukta TV

JKT yatangaza nafasi za mafunzo ya kujitolea kwa vijana 2026/27

JKT yatangaza nafasi za mafunzo ya kujitolea kwa vijana 2026/27

Nukta TV