Mikoa 10 iliyoongoza kwa watu wengi zaidi Tanzania 2025

Dar es Salaam. Mkoa wa Dar es Salaam umeendelea kuongoza kwa kuwa na idadi kubwa zaidi ya watu Tanzania Bara mwaka 2025, ukikadiriwa kuwa na wakazi milioni 5.87, ukifuatiwa na Mwanza yenye milioni 4.12 na Tabora yenye milioni 3.78.
Mikoa mingine iliyoongoza kuwa na idadia ya watu wengi kwa mujibu wa Takwimu za Msingi za mwaka 2025 zilizotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) June 15, 2026 Morogoro, Dodoma, Geita, Kagera, Tanga, Kigoma na Mara.
Ongezeko la idadi ya watu katika mikoa hiyo linaonesha kuendelea kukua kwa mahitaji ya huduma za kijamii na kiuchumi, ikiwemo afya, elimu, maji na makazi.