BoT: Miaka saba jela ukikutwa na fedha bandia

November 6, 2026 7:04 pm · Kelvin Makwinya
Share
Tweet
Copy Link
  • Kwa mujibu wa Kifungu cha 348 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, mtu anayenunua, kupokea au kumiliki noti bandia huku akijua kuwa ni bandia, anatenda kosa linaloweza kumfanya ahukumiwe kifungo cha hadi miaka saba jela.

Dar es Salaam. Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imeonya vitendo vya utengenezaji, usambazaji na matumizi ya fedha bandia, ikisisitiza kuwa vitendo hivyo ni kinyume cha sheria za nchi na wahusika watachukuliwa hatua za kali za kisheria.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 348 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, mtu anayenunua, kupokea au kumiliki noti bandia huku akijua kuwa ni bandia, anatenda kosa linaloweza kumfanya ahukumiwe kifungo cha hadi miaka saba jela.

Shadrack Mapunda, Ofisa wa BoT kutoka Kurugenzi ya Sarafu amewaambia wanahabari hivi karibuni kuwa ni muhimu kwa kila mwananchi kujifunza na kuwa na elimu ya msingi ya kutambua alama za usalama kwenye noti ili kubaini fedha bandia kabla ya kuzipokea.

Amesisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuwa waangalifu wanapopokea fedha, akieleza kuwa hata mtu ambaye hakutengeneza fedha hizo anaweza kuwajibika kisheria endapo atakutwa nazo.

“Kama ukimwazima begi rafiki yako, akarudisha lina madawa ya kulevya ndani, hata kama hukukagua ukajua, wewe ndiye utakayekamatwa kwanza,” amesema Mapunda.

Unavyoweza kutambua fedha bandia

Unaweza kutambua uhalali wa noti za Tanzania kwa kuchunguza alama zake za kiusalama zilizowekwa mahsusi kuzuia utengenezaji wa fedha bandia. 

Alama hizo ni pamoja na picha fiche (watermark), uzi wa usalama (security thread), alama zinazokutana pande zote za noti (see-through feature), maandishi au picha zinazobadilika mwonekano noti inapoinamishwa pamoja na alama zinazoweza kutambuliwa kwa mguso.

Kwa mujibu wa Mapunda, ili kufanya hivyo, unaweza kuiweka noti kwenye mwanga na kuchunguza alama zake. Noti halali inapaswa kuonesha picha iliyofichika ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, pamoja na thamani ya noti husika. 

Kwa mujibu wa Kifungu cha 348 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu, Sura ya 16, mtu anayenunua, kupokea au kumiliki noti bandia huku akijua kuwa ni bandia, anatenda kosa linaloweza kumfanya ahukumiwe kifungo cha hadi miaka saba jela. Picha | BoT

Aidha, alama zilizochapishwa pande zote mbili za noti zinapaswa kukutana na kuunda namba kamili inayoonesha thamani ya noti.

Pia, noti inapogeuzwa kuelekea pande tofauti, baadhi ya alama hubadilika mwonekano au rangi, ikiwemo alama yenye picha ya twiga inayobadilika kutoka dhahabu kwenda kijani. 

Pamoa na hayo, noti halali pia huwa na maandishi na picha zilizochapishwa kwa ubora unaoonekana wazi, pamoja na maandishi maalumu yaliyoinuka ambayo yanaweza kutambuliwa kwa kuyagusa. 

Mapunda amewashauri wananchi  kutotegemea alama moja pekee, bali kukagua alama kadhaa kabla ya kupokea fedha na ikiwa mfanyabiashara ana desturi ya kupokea fedha nyingi kwa wakati mmoja anaweza kutumia mifumo ya malipo ya kidijitali ili kupunguza hatari ya kupokea fedha bandia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Masoko & Zaidi
Loading…
No recent matches
No upcoming matches
/
No matches found for this filter
No forex gainers today
No forex losers today
Forex rates unavailable
6 Nov, 2026 · TZS
No gainers today
No losers today
6 Nov, 2026
No active movers today

Inaendeshwa na Nukta AI

Follow us on TikTok

Nukta Habari

FOLLOW NOW
Subscribe to our channel

Nukta TV

SUBSCRIBE NOW
BEI YA MAFUTA DAR | Sh10,000 kununua lita 2.44 za petroli, 2.42 za dizeli

BEI YA MAFUTA DAR | Sh10,000 kununua lita 2.44 za petroli, 2.42 za dizeli

Nukta TV

Namna Rais Samia alivyoshiriki kwenye Uchaguzi Mdogo, Jimbo la Chamwino

Namna Rais Samia alivyoshiriki kwenye Uchaguzi Mdogo, Jimbo la Chamwino

Nukta TV

Ndejembi: Wanachamwino wameona kwa macho, mrithi wangu ataendeleza kasi ileile

Ndejembi: Wanachamwino wameona kwa macho, mrithi wangu ataendeleza kasi ileile

Nukta TV